Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa awasili Moshi kuhudhuria siku ya amani kimataifa

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipokea hua wa Amani (Peace dove), alipowasili kwenye kileke cha maadhimisho ya siku ya amani Duniani, ambapo kitaifa inafanyikia mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro

Muktasari:

Kwa mara ya kwanza, siku ya amani Kimataifa iliadhimishwa Septemba 21 mwaka 1982 baada ya Baraza la Umoja wa Mataifa kutangaza siku hiyo kuwa ndio siku maalumu ya kukumbushana juu ya kuimarisha maadili ya amani.

Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasili mkoani Kilimanjaro kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani duniani ambayo inafanyika Kitaifa mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Maadhimisho hayo ambayo yanabebwa na kauli mbiu ya “amani yetu, maendeleo yetu" kwa mara ya kwanza, siku ya amani kimataifa iliadhimishwa Septemba 21 mwaka 1982 baada ya Baraza la Umoja wa Mataifa kutangaza siku hiyo kuwa ndiyo siku maalum ya kukumbushana juu ya kuimarisha maadili ya amani.

Viongozi  mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere pamoja na mwenyeji wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, viongozi wa dini mbalimbali pamoja na viongozi  kutoka Umoja wa Mataifa (UN) wamehudhuria maadhimisho hayo.

Baada ya kuwasili Waziri Mkuu alipokea matembezi ya amani na kisha viongozi dini walifanya maombi kuombea amani kwa Taifa katika ukumbi wa Kuringe uliopo mjini Moshi.