Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majaliwa awataka viongozi kulinda amani

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya amani duniani ambayo kitaifa yamefanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Muktasari:

  • Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka watendaji na viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawajibika kulinda amani na kubaini viashiria vya uvunjifu wa amani na kuvidhibiti kabla ya kuleta madhara.

Moshi. Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka watendaji na viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawajibika kulinda amani na kubaini viashiria vya uvunjifu wa amani na kuvidhibiti kabla ya kuleta madhara.

Majaliwa ameyasema hayo leo Jumatano Septemba 21, 2022, mjini Moshi mkoani Kilimanjaro, wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya amani duniani.

"Kuhusu amani naweza kusema maneno mengi sana, najua wajibu wetu sisi kama viongozi wa serikali na hasa sisi ambao tunamsaidia Rais, kwenye ajenda yake ya kuitaka nchi hii iwe imetulia, mimi na wenzangu, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, makatibu wakuu na wengine, sote tusimame kwa pamoja kuhakikisha kwamba nchi hii tunaendelea kuifanya kuwa ya amani"

"Pale itakapotokea kwenye maeneo tuliyoaminiwa na kukabidhiwa dhamana na Rais, halafu kunatokea vurugu na sisi tupo, tutakuwa hatujamtendea haki, kwa hiyo nitoe wito kwa watendaji wote serikalini kuhakikisha kila siku kama kuna viashiria, tunaviwahi, tunaviondoa".

Majaliwa amesema kuwa amani ni kitu muhimu cha kuzingatia katika ajenda za maendeleo endelevu ya nchi hivyo kuwataka watanzania wote kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani na wale wote wanaotaka kuchafua amani ya nchi.

"Kama kweli tunaangalia kwenye vyombo vya hanbari namna wenzetu wnavyoteseka akina mama, watoto na wazee wasiokuwa na uwezo wa kukimbia sisi Watanzania lazima tujipange kudhibiti kwa yeyote anayetaka kuchafua amani ya nchi yetu" amesema Majaliwa

"Ndugu zangu amani ni kama yai ni rahisi sana kuvunjika ni lazima litunzwe kulingana na umuhimu wake. Leo kuna nchi ambazo haziwezi kukaa pamoja hivi lakini leo tuko hapa na tuna matumaini makubwa, nchi nyingine haiwezekani, jukumu la kuidumisha na kuilinda amani yetu ni ajenda yetu,"

Mwakilishi mkaazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Mulisic ameipongeza Tanzania kuwa kinara wa kutunza amani barani Afrika.

"Sehemu yoyote ambayo hakuna amani, hakuna maendeleo yanayoweza kufanyika hali ambayo huchochea kudorora kwa uchumi, hivyo niipongeze Tanzania kwa kuwa nchi ya kisiwa cha amani, endeleeni kuitunza na kuilinda amani hii kwa maendeleo ya nchi" amesema