Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Majonzi yagubika wakiwapokea wazazi waliofiwa na watoto wanne

Baadhi ya majirani wa familia ya Mzee Hashim Msuya iliyopoteza watoto wanne katika ajali  ya gari iliyotokea Mbwewe mkoani Pwani Agosti 2,2023 walipofika nyumbani kwake Uzunguni Kata ya Tambukareli jijini Dodoma kumfariji.

Muktasari:

  • Mzee Hashim Msuya na mkewe Lilian leo wamepokelewa na majirani zao wakitokea jijini Dar es Salaam walipokuwa katika msiba wa watoto wao wanne waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea Agosti 2, 2023 kwenye eneo la Mbwewe mkoani Pwani.

Dodoma. Familia iliyopoteza watoto wanne katika ajali ya gari katika eneo la Mbwewe mkoani Pwani leo imepokelewa kwa majonzi na majirani waliofika nyumbani kwao Uzunguni, Kata ya Tambukareli jijini Dodoma.

Familia hiyo ya Hashim Msuya ilipoteza watoto wanne Agosti 2, 2023 katika ajali ya gari katika eneo la Mbewe mkoani Pwani, wakati wakitokea jijini Dar es Salaam kuelekea Mwanga kwenye msiba wa mdogo wao ambaye ni mtoto wa baba yao mdogo wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Sia Msuya, Neech Msuya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Benki ya ABSA, Dk Norah Msuya (Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe) na Diana Msuya.

Majirani hao walikwenda kuwapokea katika uwanja wa ndege wa jijini Dodoma leo Jumanne Agosti 21, 2023 na kwenda nao nyumbani ambapo walikutana na majirani wengine walikuwa wakiwasubiria nyumbani kwao Uzunguni jijini Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi nyumbani kwake, Mzee Msuya amesema amewashukuru Watanzania, viongozi wa dini na majirani kwa mshikamano, upendo na faraja waliyoionyesha katika kipindi chote cha msiba wa watoto wake.

Pia alivishukuru vyombo vya habari hasa Mwananchi kwa kuifahamisha dunia juu ya masuala yalikuwa yakiendelea kwenye msiba tangu ulipotokea Agosti 2, mwaka 2023. 

“Sikutarajia kupata faraja kama niliyoipata hiyo lakini pia hata baada ya msiba kumalizika marafiki wa wanangu walikuwa hawakauki nyumbani kwa mwanangu (Dar es Salaam) hadi aliporejea Dodoma,”amesema.

Amemshukuru majirani, Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali kwa kuguswa na tatizo hilo na hivyo kutoa msaada wa matibabu kwao.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Salmin ambaye ni jirani yake Mzee Msuya, Edna Ndejembi amesema japokuwa familia hiyo ilishamaliza msiba lakini ni watu wanaohitaji faraja kubwa kutoka kwa wakazi wa Dodoma kutokana msiba uliomkuta.

“Hii ni nyumba amabayo waliwapa watoto na kuwakuzia wanaporudi na kufikiri wamebaki pekee yao ni jambo ambalo linazidi kuwapa uchungu. Ninawaomba majirani wenzangu tuendelee kuwafariji. Hata kama si kwa kutoa chochote lakini kwa kufika tu na kuwajulia hali,” amesema.