Makonda amuaga Magufuli Uwanja wa CCM Kirumba

Muktasari:
- Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameungana na wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa ya jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba.
Mwanza. Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameungana na wakazi wa Jiji la Mwanza na mikoa ya jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli katika uwanja wa CCM Kirumba.
Makonda aliyeondoka kwenye wadhifa huo baada ya kuomba kugombea ubunge Kigamboni ameonekana uwanjani hapo akiwa ameongozana na waombolezaji wengine akiwa amevalia kaunda suti nyeusi..
Kabla ya kuwa mkuu wa Mkoa, Makonda aliyeibukia kwenye uongozi wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM) alikuwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Baada ya Makonda kujitosa kuwania ubunge na kushika nafasi ya pili katika kura za maoni ndani ya CCM, Magufuli alimteua Aboubakar Kunenge kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.