Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malalamiko ya dhuluma yatawala ziara ya Dk Mwigulu

Muktasari:

  • Malalamiko hayo yamewasilishwa na wananchi kutoka ndani na nje ya mkoa huo wa Mara

Musoma. Malalamiko ya wananchi kuhusu kudhulumiwa mali na watu wenye mamlaka au uwezo wa kifedha ya-mejitokeza katika ziara ya Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, iliyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, huku wananchi wakiwasilisha kero mbalimbali wakitaka zipatiwe ufumbuzi.

Malalamiko hayo yamewasilishwa leo, Jumamosi, Julai 4, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Suguti, wilayani Musoma, baada ya wananchi kupata nafasi ya kueleza changamoto zao kwa Waziri Mkuu.

Wananchi kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Mara wameeleza kuwa wameamua kufikisha malalamiko yao katika mkutano huo wakiamini yatafanyiwa kazi na hati-maye kupata haki zao.

Mkazi wa Kijiji cha Suguti, Kaswamila Kaswamila, amesema Desemba 2024 alizuiwa kuuza nyama ya ng'ombe alio-wachinja kwa madai ya kukosa vibali, hali iliyosababisha hasara baada ya nyama hiyo kuharibika.

"Baada ya kunizuia, nilifanya ufuatiliaji bila mafanikio hadi ile nyama ikaoza. Licha ya kufikisha suala hili kwa Mku-rugenzi na DC, hadi sasa sijapata fidia kwa sababu sikuweza kuiuza ikafikia hatua ya kuharibika," amesema.

Hata hivyo, Dk Mwigulu alimpa nafasi ya kuzungumza mwenyekiti wa kijiji hicho, Sadiki Chiguma ambaye ames-ema alizuia uuzwaji wa nyama hiyo baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa ofisa mifugo wa kata, aliyesisitiza kuwa, kila anayechinja na kuuza nyama lazima awe na vibali ili kudhibiti wizi wa mifugo.

"Maelekezo haya yalitokana na changamoto ya wizi wa mifugo. Ili kudhibiti hali hiyo, wafanyabiashara wote walitakiwa kuwa na vibali na vielelezo vinavyoonesha wamenunua wapi na rangi ya ng’ombe wake au mfugo huo," amesema.

Mkazi wa Kijiji cha Chirorwe, Mashauri Machumu amedai mwenyekiti wa kijiji amemnyang’anya mama yake eneo la ardhi alilokuwa akilitumia tangu mwaka 1979 na kuligawa kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu bila ridhaa ya famil-ia.

Amesema licha ya jitihada za kufuatilia kupitia viongozi mbalimbali, bado hawajapata muafaka, hivyo amemuomba Waziri Mkuu kuingilia kati ili mama yake apate haki yake.

"Maeneo yale ni ya mama yangu, lakini wanaonufaika ni wengine. Tunaomba msaada ili apate haki yake," amesema.

Mkazi wa Mkoa wa Geita, Laurencia Makanza amelalami-ka kudhulumiwa Sh10 milioni alizokuwa amemkopesha mtu kwa ajili ya shughuli za uchenjuaji wa dhahabu, fedha am-bazo hadi sasa hazijarejeshwa licha ya makubaliano ya kisheria.

"Waliingia makubaliano mbele ya wakili kwamba irejeshwe ndani ya mwezi mmoja na nusu, lakini hadi sasa sijalipwa," amesema.

Kwa upande wake, Emmanuel Omoso mkazi wa Bugwema amesema yeye na wenzake wanne walipoteza ng’ombe 360 baada kutapeliwa na mtu mmoja ambaye kesi yake ilif-ikishwa mahakamani na kuamriwa kurejesha mifugo hiyo, lakini hukumu haijatekelezwa.

"Anakamatwa na kuachiwa licha ya hukumu ya Mahakama. Tunaomba msaada ili haki itendeke," amesema.

Mkazi wa Mwanza, Eric Mathew amesema mpangaji wake alighushi nyaraka kuonesha kuwa anamdai Sh48 milioni.

Amesema mpangaji huyo alifungua kesi katika baraza la nyumba ambalo liliamuru kuwa anatakiwa kumlipa Sh48 milioni pamoja na riba ya asilimia 30.

Amesema waliamua kukata rufaa Mahakama Kuu iliyoten-gua hukumu hiyo lakini tangu hukumu hiyo itenguliwe mwaka 2023, hadi sasa mtu huyo amegoma kuondoka kwenye nyumba hiyo.

Naye mkazi wa Arusha, Zubeda Kasoga amesema yeye pamoja na wafanyakazi wenzake 350 waliokuwa wakifan-yakazi Kiwanda cha Fiber Board Africa walitakiwa kulipwa mafao yao kutokana na kiwanda hicho kubinafsishwa mwaka 1998 lakini hadi sasa bado hawajapata mafao hayo.

Kutokana na malalamiko hayo, Waziri Mkuu Mwigulu ameelekeza mamlaka mbalimbali kushughulikia malalamiko hayo kulingana na yalipoelekezwa.

Miongoni mwa waliolekezwa kushughulikia malalamiko hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Juma Chikoka, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda na watu wa ofisi ya Wa-ziri Mkuu na mamlaka zingine.