Mama ajifungulia kanisani baada ya kumuomba Mungu mtoto wa kike

Mama ajifungulia kanisani baada ya kumuomba Mungu mtoto wa kike

Muktasari:

Mkazi wa mtaa wa Kilimahewa kata ya Bulangwa wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita, Justina Lukilisha amejifungua mtoto nje ya kanisa la Ufunuo mjini Ushirombo baada ya kuumwa unchungu ghafla.

Bukombe. Mkazi wa mtaa wa Kilimahewa kata ya Bulangwa wilaya ya Bukombe mkoa wa Geita, Justina Lukilisha amejifungua mtoto nje ya kanisa la Ufunuo mjini Ushirombo baada ya kuumwa unchungu ghafla.

Lukilisha amejifungua mtoto wa kike leo Jumapili Januari 3, 2021 akiwa kwenye ibada akidai kuwa hakutegemea uchungu ungemshika kwenye ibada.

Lukilisha anasema anamshukuru Mungu kwa kuwa alifika kwenye ibada kwa ajili ya kumuomba Mungu ili apate mtoto wa kike.

Mkunga toka kijiji cha Nyag'holongo wilaya ya Mbogwe, Letisia Komka ambae pia ni muumini wa kanisa hilo amesema mama huyo amejifungua salama.

Mumini wa kanisa la Ufunuo, Elizabeth Ernest amesema tangu aanze kusali hajawahi kuona mtu anajifungulia kanisani akiamini kuwa huo ni mpango wa Mungu.

Naye, Penina Jemes amesema Jumapili ya kwanza baada ya mwaka mpya ni ya neema kwa mama mjamzito kujifungua mtoto wa kaki kanisani.

Askofu wa Kanisa la Ufunuo jimbo la Geita, Heryyabwana Majebele amesema mama huyo alikuja na hitaji kubeba mimba tena akiitaji mtoto wa kike na leo kabla ya kuingia kanisani alisema tu anajisikia uchovu lakini ghafla aliumwa uchungu.

Askofu Majebele amesema kwa sasa mama huyo ameenda hospitali ya wilaya ya Bukombe kwa ajili huduma zingine na anaendelea vizuri.