Mamba ‘watoa roho za watu’ wauawa Ziwa Victoria

Wananchi wkiwa katika picha ya pamoja na mamba waliouwawa wakisadikiwa kuua watu Ziwa Victoria

Buchosa. Mamba wawili waosadikiwa  kushambulia watu Ziwa Victoria wameuawa katika Kata ya Nyakasasa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Mkoa wa Mwanza.

Zoezi la kuwanasa mamba hao limeendeshwa na maofisa  Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri)  iliyoko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mamba hao ambao wamenaswa leo Ijumaa Machi 17, 2023 na hivi karibuni walimshambulia mtu mmoja kisha kupoteza maisha kwenye Kijiji cha lugata kisiwani Kome.

 Zoezi la kuwaua mamba hao linaongozwa ofisa kutoka maofisa wa Tawiri, Mohamed Mpoto amesema baada ya kusikia kilio cha wananchi wa Buchosa wamepiga kambi Kisiwa cha Kome kuwavuna mamba hao sambamba na kutoa elimu kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa Kisiwa cha Kome wamepongeza hauta ya Serikali kutumia  ya maofisa wanyapori kuvuna mamba hao ambao walikuwa ni kero kwa wananchi.

Endelea kufuatia mitandao ya kijamii ya Mwananchi kwa habari zaidi.