Manyara yakithiri vitendo vya ukatili

Kiteto. Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kiteto, Mosi Sassy amesema vitendo vya jinai kama vile ubakaji, ulawiti, kutoa mimba kwa wanafunzi na mauaji havina suluhu ni kosa kisheria hivyo  vikiendelea vitaleta madhara kwa jamii.

 Akizungumza mbele ya wadau wa sheria wakiwemo wanafunzi 1,143 wa Shule ya Sekondari Kiteto leo Januari 23,2023, Hakimu Mosi Sassy amesema kukithiri kwa vitendo hivyo ni kutokana na wengi wa wananchi kufanya suluhu vitendo vya kijinai.

"Ndani ya jamii kuna baadhi ya watu wanasuluhisha vitendo vya ubakaji, ulawiti na hata mimba kwa wanafunzi, hili ni kosa kisheria...Tukiendelea kufumbia macho haya madhara zaidi tutaendekea kuyaona na yataendelea," alisema Sasi.
Alisema sheria iko wazi na kila mara elimu imekuwa ikitolewa na hapa tunaendelea kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii...Tuache kufanya suluhu ya mambo ya kijinai alisema Sassy.
Kwa upande wa mawakili, Ibrahimu Mohamed Massawe, na Pastor Kong'oke walieleza wanafunzi hao wa Kiteto Sekondari kuwa baadhi yao wamekuwa kikwazo katika kesi za mimba kwa kuharibu ushahidi miongoni mwao wanapopatikana na mimba.

"Mwanafunzi anapopata mimba na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa mara ya kwana anamkana aliyempa mimba wakati awali alimtaja jambo ambalo linafanya kesi hizi sasa kutoshughulikiwa kikamilifu kwa kuharibiwa na wahusika," alisema Wakili Brahimu.
Wakili Kong'oke katika elimu hiyo alisema masuala ya suluhu ni kama vile mkulima kuingia eneo la ardhi ya mwenzake kwa kulima bila kujua au kutojua hivyo hapo wanaweza kufanya suluhu," alisema Kong'oke.
Nao baadhi ya wanafunzi wa Kiteto Sekondari katika elimu hiyo walisema ndani ya jamii kuna baadhi ya watu wanapotosha sheria vijiini huku ikieleweka kwao kuwa wako sahihi na wengine kuiga hayo wakidhani wako sahihi.
Walisema ili nao waweze kuepukana na mkono wa sheria  elimu zaidi iwafikie haswa watu wa vijijini ambao wao wamekuwa hawapati uelewa mzuri wa sheria na kujikuta wakiadhibiwa kwa kutojua, walisema.