Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maofisa mifugo 3,018 kuhudumia wafugaji kidigitali

Mshauri wa kiufundi wa FAO aliyemwakilisha Mwakilishi mkazi wa FAO, Monday Ahonsi akikabidhi moja ya vifaa vya Tehama kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Mhina jana jijini Dodoma.

Muktasari:

  • Kupitia mfumo wa M-Kilimo, Ugani Kiganjani (EMA-I) na MIMIS wafugaji wamekuwa wakipata huduma za ushairi kuhusu afya za wanyama na masoko ya mifugo yao.

Dar es Salaam. Serikali imesajili jumla ya maofisa mifugo 3,018 katika jukwaa la M-Kilimo linalowasiliana na wafugaji kupata huduma za ugani zikiwamo za afya na masoko ya mifugo.

Hayo yameelezwa jana Septemba 12 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Mhina alipokuwa akipokea vifaa vya Tehama kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kupokea na kupiga simu za kutoa huduma za ugani kwa wafugaji kutoka kwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi na FAO wamekuwa wakishirikiana na kutoa huduma za kdigitali tangu mwaka 2020.

“Kati ya mwaka 2020 hadi 2023, FAO imeisaidia Wizara kuendeleza utoaji wa ujumbe mfupi ili kusaidia kufikisha, udhibiti na kuriporti magonjwa ya kipaumbele na magonjwa yanayovuka mipaka ya wanyama na masuala ya lishe za wanyama

“Ujumbe huo husambazwa kwa kutumia mfumo wa kidigitali wa FAO (DSP) uitwao Ugani Kiganjani kwa wakulima,” amesema.  

Amesema pia FAO imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kuwajengea uwezo maofisa mifugo ya jinsi ya kugundua hatari za kiafya za wanyama na kulinda afya zao kwa kutumia jukwaa la matumizi ya simu (EMA) katika halmashauri 114 nchini.

“Mfumo wa wizara wa M-Kilimo, Ugani Kiganjani, (EMA-I) na MIMIS imeonyesha mafanikio katika kutoa huduma za Serikali kidigitali. Pia jukwaa hilo hutoa vifaa vya ugani kwa maofisa zikiwamo shajara kwa ajili ya kuweka taarifa,” amesema.

Akifafanua utendaji kazi wa mfumo huo, amesema maswali ya wananchi hupokelewa na wizara na maofisa kwa ajili ya watumiaji.

“Ndani kuna kundi la WhatsApp linalowakusanya maofisa wa wizara, timu ya Tehama na waendesha mifumo ambako masuala hutumwa na kutatuliwa kwa wakati,” amesema.

Vifaa vilivyotolewa na FAO ni pamoja na kompyuta saba, skrini ya nchi 65 na spika za masikioni saba vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh26.34 milioni.

“Ni matumaini yangu kuwa, msaada huu utaongeza thamani katika kuanzishwa kwa kituo cha kupiga na kupokea simu, japo kuna upungufu katika miundombinu na uwezo wa maofisa husika katika kutoa huduma kwa ufanisi,” amesema Dk Mhina.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, mshauri wa kiufundi wa FAO aliyemwakilisha Mwakilishi mkazi wa shirika hilo katika shughuli hiyo, Monday Ahonsi, amesema wametoa vifaa hivyo baada ya kupata maoni ya wizara hiyo.

“Kwa siku za hivi karibuni, Tanzania imeshuhudia ongezeko la matumizi ya huduma simu na intaneti katika kilimo, mifugo na uvuvi kutokana na kuongezeka kwa mtandao wa simu za mkononi katika maeneo ya vijijini.

“FAO inaamini kwamba vifaa vikitumika kama viulivyokusudiwa vitaondoa changamoto ya kukosekana kwa huduma za ugani kwa wafugaji na uvuvi na kuongeza upatikanaji wa chakula,” amesema.

Amesema ushirikiano kati ya wizara na FAO unalenga kusadia nchi kutumia fursa za kilimo kupunguza umasikini na kuongeza malengo la uchumi jamii na kuwezesha wafanya maamuzi kuzipa kipaumbele hatua zinazotakiwa kuchukuliwa na kuhamasisha uwekezaji.

“Ndiyo maana tunatakiwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha kwamba kuna uendelevu wa matumizi ya huduma za kilimo cha kigitalikwa ajili ya jamii zikiwamo za wafugaji, wavuvi wa samaki na wavuvi,” amesema.