Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Marais wa nchi 10 kumuaga Magufuli Dodoma

Marais wa nchi 10 kumuaga Magufuli Dodoma

Muktasari:

  • Marais  zaidi ya 10 wa mataifa mbalimbali duniani wamethibitisha kuhudhuria shughuli ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli itakayofanyika kesho Dodoma.

Dar es Salaam. Marais  zaidi ya 10 wa mataifa mbalimbali duniani wamethibitisha kuhudhuria shughuli ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli itakayofanyika kesho Dodoma.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abasi amesema leo Machi 21, 2021 kuwa hadi sasa ana orodha ya zaidi ya marais 10 na kuahidi kuweka wazi majina na nchi zao mchana wa leo.

Magufuli alifariki dunia Machi 17 kutokana na maradhi ya moyo.

Rais huyu wa awamu ya tano anatarajiwa kuzikwa Machi 26 nyumbani kwao Chato mkoani Geita.