Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matinyi: Kuweka wazi mkataba bandari ni kuanika siri

Muktasari:

  • Wakati kilio cha watu wengi ikiwa ni kutaka mkataba wa miaka 30 wa uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam uliosainiwa kati ya DP World na Serikali kuwekwa wazi, Msemaji wa Serikali amesema kuweka wazi mkataba ni sawa na kuanika siri za uwekezaji.

Dar es Salaam. Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema, kuwekwa wazi kwa mkataba wa uwekezaji wa bandari ya Dar es Salaam ni sawa na kuweka hadharani siri za bandari na zile za mwekezaji.

Hiyo ni kutokana na kile alichoeleza kuwa Bandari ya Dar es Salaam inashindana na bandari nyingine ikiwemo ile ya Mombasa.

Ametoa kauli hiyo leo Oktoba 25 wakati akichangia maoni yake katika Mwananchi Space iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) kujadili mada isemayo 'Mkataba bandari umekidhi matarajio ya wananchi?'

Maoni yake pia yanakuja ikiwa ni siku nne tangu Serikali kusaini mkataba na Kampuni ya DP World (HGA) kwa ajili ya kuendesha baadhi ya gati za Bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 30.

Akizungumza katika Mwananchi Space, Matinyi amesema mkataba wa kibiashara ni siri na kuweka hadharani mkataba huo kunaweza kutishia wawekezaji wengine.

"Wawekezaji wengine watasema ukienda Tanzania unaenda kumwaga siri za kampuni na wataogopa kuja, hatutashawishi wafanyabiashara wengine kuja kuwekeza," amesema Matinyi.

Amesema mitambo inayokwenda kuwekwa katika eneo hilo mmoja ni dola 25 milioni (zaidi ya Sh65.5 bilioni) na Serikali ya sasa imenunua mitatu ambapo mmoja umekwensa kufungwa bandari ya Mtwara wakati Bandari ya Mombasa wanayo 20.

"Sasa tuchukue 20 tuzidishe kwa dola 25 milioni  tuone inakuja ngapi, huu siyo uwezo wetu wa kufanya vitu ghafla hivi," amesema Matinyi.

Akizungumzia namna ilivyokuwa, Matinyi amesema gati nne hadi saba ambalo ni eneo la makontena lilipokuwa chini ya  Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), lilikuwa likizidiwa makontena mara tatu hadi nne na kampuni binafsi ya Kimataifa ya Kuhudumia Makontena Tanzania (TICTS) iliyokuwa ikiendeaha gati namba nane hadi 11.

"Meli ilipokuja ilichagua kwenda kwenye magati yale, iko radhi isubiri kidogo ili uhudumiwe kule kwa sababu ya ubora wa huduma. Sasa ili tufikie hapo na kupita ndiyo maana gati namba nne hadi saba inakwenda kuwa chini ya DP World ili tuweze kufikia kiwango hicho," amesema Matinyi.

Amesema hata  ambao walikuwa wakiizidi TPA kwa kati ya mara tatu hadi nne lakini bado tathimini ilionyesha walikuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na mkataba wao haukufika mwisho kwani ulikuwa unaishia mwaka 2025 lakini umeishia mwaka 2022.

"Na hili gati namba nane hadi 11 TPA inatafuta mwekezaji mwingine aje akodishiwe aendeshe," amesema Matinyi.

Amesema bandari inashindana na bandari nyingine ikiwemo Beira (Msumbiji) na Mombasa (Kenya), hivyo kutaka mkataba wa bandari ya Dar es Salaam uwe wazi maana yake bandari haitakuwa salama.

"Pia wawekezaji wengine wataweza kutishika kwamba ukienda Tanzania unaenda kumwaga siri za kampuni na hivyo wawekezaji wengine kuogopa kuja," amesema.