Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili wa Raila wakataa uamuzi wa mahakama

Muktasari:

Timu ya mawakili wa aliyekuwa mgombea urais wa Kenya Raila Ondinga wamesema wameupokea lakini hawaukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu ya nchi hiyo iliyotupilia mbali maombi yao ya kupinga matokeo ya uchanguzi uliompa ushindi William Ruto.

Dar es Salaam. Timu ya mawakili wa aliyekuwa mgombea urais wa Kenya Raila Ondinga wamesema wameupokea lakini hawaukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu ya nchi hiyo iliyotupilia mbali maombi yao ya kupinga matokeo ya uchanguzi uliompa ushindi William Ruto.

Leo Jumatatu Septemba 5, 2022, Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali maombi ya kikatiba yalifunguliwa na Raila Odinga kupinga ushindi wa Ruto.

Baada ya uamuzi, kiongozi wa jopo la mawakili Ondinga, wakili mwandamizi James Orengo amewaambia waandishi wa habari muda mfupi baada ya uamuzi huo kuwa uamuzi wa mahakama hiyo ulikuwa wa kiitikadi zaidi kuliko kisheria.

Kwa mujibu wa sheria tunalazimika kuupokea huu uamuzi lakini nadhani ulikuwa wa kiitikadi zaidi. Tunaupokea lakini hatukubaliani nao,” amesema Orengo.

Wakili huyo alisema wao walitaka ukaguzi wa kina wa vifaa na nyaraka zote zilizotumika katika uchaguzi lakini mahakama haikujikita katika kulifafanua hilo.

Jaji Mkuu Martha Koome metupilia mbali rufaa ya Raila na wenzake akisema waleta maombi wenzake wameshindwa kuthibitisha kuwa kulikuwa na udanganyifu na uchakachuaji wakati wa mchakato wa kuelekea uchaguzi, siku na baada ya kupiga kura.

Odinga (77), mwanasiasa mkongwe ambaye aligombea huku akiungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta amepinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9, akiyaita ‘upotoshaji.’

Alishindwa na Ruto kwa kura 230,000 tu chini ya asilimia mbili tu alizohitaji

Uamuzi huo unamfanya Ruto kuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Kenya kufuatia uchaguzi uliokuwa na upinzani mkali. Anatarajiwa kuapishwa Jumanne ijayo.

Katika matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Wafula Chebukati Agosti 15, 2022, Dk William Ruto alishinda kwa kura 7,176,142 (asilimia 50.49 ya kura) na Raila Odinga akafuatiwa kwa kura 6, 942, 930 (asilimia 48.85). wangombea wengine wawili hawakufikisha asilimia moja ambapo David Waihiga alipata asilimia 0.23 % huku George Wajackoyah akipata asilimia 0. 44.