Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawakili wa utetezi walivyombana shahidi kesi ya kina Mbowe

Muktasari:

  • Baada ya shahidi wa pili upande wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Justine Eliya Kaaya kutoa ushahidi wake alihojiwa na mawakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya na John Mallya.


Dar es Salaam. Baada ya shahidi wa pili upande wa Jamhuri katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, Justine Eliya Kaaya kutoa ushahidi wake alihojiwa na mawakili wa utetezi Jeremiah Mtobesya na John Mallya.

Kaaya, ambaye alikuwa mpiga picha wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ametoa ushahidi huo jana Jumatano Oktoba 21, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu.

Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano hayo:

Wakili Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema mbali na ushahidi wa mdomo uliyoutoa hapa mahakamani, kuna udhibitisho wowote umetoa kama kweli ulikuwa unafanya kazi kwa Sabaya?

Shahidi: Hicho nilichoongea ndio sahihi.

Wakili: Kuna udhibitisho wowote umetoa?

Shahidi: Sijaulizwa chochote wakati naongozwa kutoa ushahidi.

Wakili: Umesema mlikuwa mnawasiliana na mtu uliyemtaja kwa jina la Mbowe kwa njia ya WhatsApp, je umetoa udhibitisho wowete hapa mahakama kuonyesha kuwa ulikuwa na mawasiliano nae?

Shahidi: Sio jukumu langu kutoa, wapo wahusika.

Wakili: Labda anayehusika ni nani kwa uelewa wako?

Shahidi: Siwezi kujua.

Wakili: Tangu mkutane na Mbowe zaidi ya mara tatu hadi unachukuliwa maelezo ya onyo ni muda gani umepita?

Shahidi: Swali uliloniuliza sio sahihi maana siwezi ku-calculate (kuhesabu).

Wakili: Tangu mlipokutana na Mbowe mpaka sasa ni zaidi ya muda gani?

Shahidi: Mwaka mmoja na miezi mitatu.

Wakili: Isaidie mahakama. Una uhakika kile ulichokisema wakati unachukuliwa maelezo na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Swilla, ndicho ulichokisema hapa mahakamani?

Shahidi: Ndio.

Wakili: Kuna ulichopunguza?

Shahidi: Hapana.

Wakili: Kuna sehemu yoyote katika ushahidi wako ulisema wewe ulishakuwa mwanasiasa?

Shahidi: Hapana.

Wakilii: Kwa hiyo wewe sio mwanasiasa?

Shahidi: Hapana, sio mwanachama wa chama chochote.

Wakili: Lini ulikuwa mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi?

Shahidi: Sijawahi kuwa mwanachama.

Wakili: Hakuna kiongozi yoyote wa kisiasa aliyekuja kukutembelea gerezani?

Shahidi: Hakuna.

Wakili: Hakuna wakati wowote ule uliandika barua ukiwa gerezani, ukiomba viongozi wa kisiasa wakusaidie kutoka katika hiyo kesi?

Shahidi: Sijawahi kuandika.

Wakili: Ulikutana na Mbowe kwa mara ya kwanza lini? Ukiwa gerezani?

Shahidi: Tarehe 26/7/2021.

Wakili: Unakumbuka namba ya kesi iliyokuwa inakukabili Kisutu?

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili: Naweza kuwa sahihi nikitaja ni kesi namba ya Uhujumu Uchumi namba 63 ya 2020?

Shahidi: Ni sahihi.

Sehemu ya mahojiano kati ya wakili wa utetezi John Mallya na shahidi ilikuwa kama ifuatavyo.

Wakili John Mallya: Shahidi, diwani analipwa shilingi ngapi kama ana mashahara?

Kaaya: Sijui

Wakili: Analipwa shilingi ngapi posho?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Sabaya akiwa diwani alikuwa anakulipa posho kutoka katika malipo gani?

Shahidi: Halikuwa jukumu langu kujua anatoa wapi.

Wakili: Alikuwa anakulipa shilingi ngapi?

Shahidi: Shilingi laki tatu.

Wakili: Ambazo hukutaka kujua kama anazipata kihalali au anaiba.

Shahidi: Mimi nilikuwa napata haki yangu.

Kisha Wakili Mallya alimpatia maelezo yake na akamwelekeza sehemu ya kusoma ambapo aliieleza kuwa baada ya kuhitimi masomo alianza harakati za siasa na kuwa msaidizi wa Katibu wa CCM Wilaya ya Arumeru, kisha akaendelea kumhoji

Wakili: Umesema ulianza harakati za siasa na ukawa msaidizi wa Katibu wa Wilaya ambaye ni wa chama gani?

Shahidi: Chama Cha Mapinduzi

Wakili: Umemtaja Sabaya kuwa ulifanya naye kazi tangu akiwa diwani, alikuwa wa chama gani?

Shahidi: Umemtaja Daqarro, aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha (Gabriel) alikuwa wa chama gani?

Shahidi: Mkuu wa Wilaya hana chama.

Wakili: Ni sahihi Rais Magufuli alimteua Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai?

Shahidi: Ni sahihi

Wakili: Alikuwa wa chama gani?

Shahidi: Chama cha Mapinduzi

Wakili: Unamfahamu mwenyekiti wa CCM taifa kwa sasa ni nani?

Shahidi: Samia Suluhu Hassan.

Wakili: Na wa Chadema?

Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe.

Wakili: Umetaja majina ya watu waliokuwa wakitembea na Sabaya akiwemo Sylvester Nyigu, ambaye amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, unalijua hilo?

Shahidi: Nimesikia.

Wakili: Hayo majina saba uliyoyataja hapa uliyataja mwaka gani kwa huyo unayemuita Mbowe?

Shahidi: Mwaka 2018 na 2020

Wakili: Uliacha kazi kwa Sabaya mwaka gani?

Shahidi: 2018 Oktoba

Wakili: Katika maelezo yako kuna sentensi inaanza mwishoni mwa mwaka 2017 ndio niliondoka kwa Lengai Ole Sabaya na kwenda kwenda Longido. Katika ushahidi wako hapa mahakamani umesema 2018, mahakama ishike kipi na iache kipi?

Shahidi: 2018, maana 2017 Sabaya alikuwa hajateuliwa kuwa DC. Mimi niliyosema chini ya kiapo ndio sahihi, hayo labda mwandishi alikosea.

Wakili: Kwenye uthibitisho unaposema hayo ndio maelezo yangu nimeyasoma yamo sahihi unamaanisha nini?

Shahidi: Yana maana ya uthibitisho.

Wakili: Mkuu wa Wilaya analipwa mshahara shilingi ngapi?

Shahidi: Mimi sijui.

Wakili: Wewe alikuwa anakulipa shilingi ngapi?

Shahidi: Mshahara wangu ulikuwa laki tatu.

Wakili: Anakulipa kutoka wapi?

Shahidi: Mimi sifahamu.

Wakili: Hao watu saba uliowataja wasaidizi wa Sabaya walikuwa wanamsaidia kazi gani?

Shahidi: Sifahamu.

Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena leo