Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mawasiliano ya televisheni sasa kwa intaneti

Muktasari:

  • Mfumo wa intaneti hutoa maudhui ya televisheni mbashara kwa watazamaji kupitia intaneti, bila kutegemea watoa huduma wa kawaida wa nyaya au satelaiti.

Dar es Salaam. Katika kukuza maeendeleo ya Tehama, sasa wnanchi wanweza kutazama televisheni zao kupitia mitandao ya intaneti.

Hiyo ni kutokana na ongezeko la huduma ya intaneti kwa umma kwa ujumla na mwingiliano wa mifumo ya utangazaji na kidijiti.

Mfumo wa intaneti hutoa maudhui ya televisheni mbashara kwa watazamaji kupitia intaneti, bila kutegemea watoa huduma wa kawaida wa nyaya au satelaiti.

Mfumo huo umewekwa wazi leo Desemba 10, 2024 wakati kampuni ya simu za mkononi, Airtel Tanzania iilipotangaza kuingia makubalino ya kimkakati na Haier Tanzania ili kuboresha huduma za intaneti majumbani kwa Watanzania.

Ushirikiano huo utamsaidia mteja atakayenunua runinga yenye ukubwa wa nchi 50 hadi 98 atapokea kifaa cha intaneti ya 5G kutoka airtel na kifurushi cha mwezi mmoja bure, mpango huu unalenga kuwapatia watanzania muunganisho wa intaneti usio na kikomo.

Uboreshaji huo ni kuleta suluhisho bunifu, nafuu na la kuaminika kwenye soko la Tanzania, suala hilo limekuja kujibu mahitaji yanayongezeka ya teknolojia ya kisasa hasa majumbani.

Ameyazungumza hayo leo Desemba 10, 2024 Joseph Muhere, amabaye ni mkurugenzi wa biashara wa Airtel, amesema ushirikiano huo wa kimkakati na kampuni ya Haier inayojiusisha na uuzaji wa wa vifaa vya umeme utakwenda kuboresho matumizi ya intaneti na kubadilisha maisha ya watanzania.

“Tunawapa wateja wetu fursa ya kufurahia urahisi na maisha ya kisasa kwa kuanganisha mtandao wetu wakasi na kuaminika wa 5G na vifaa bunifu vya Haier, ushirkianio huu unakamilisha lengo letu la kurahisisha maisha ya wateja wetu kupitia suluhisho na bidhaa za kiditali za haili ya juu”, amaesema Muhere

Jackson Mbando, mkuu wa kitengo cha mawasiliano airtel amesema uboreshaji huo umekuja wakati mzuri ikiwa ni mwisho wa mwaka hivyo familia nyingi huwa zipo nyumbani pamoja hivyo ni wakati mzuri wa kufurahia intaneti.

“Mtandao wetu unajulikana kwa kazi nzuri unaofanya, kwa sasa tumeamua kuwafata nyumbani wateja wetu, ukizingatia huu ni mwisho wa mwaka hivyo familia nyingi huwa zipo nyumbani ni wakati wao sasa kupata intaneti yenye kasi zaidi ili kufurahia kipindi hiki kuerekea sikuu za mwisho wa mwaka,” amesema Mbando.

Mkuu wa biashara wa Haier Tanzania Ibrahim Kiongozi, ameonesha kufurahishwa na ushirikiano huo, kwani utaleta mabadiliko ya intaneti kwa watanzania hasa kwa kipindi cha hiki cha sikukuu ya chrismas na mwaka mpya.