Mawaziri watua mpaka wa Holili sakata la mahindi yaliyozuiwa

Wednesday April 07 2021
WAZIRIPIC

Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa Adolf Mkenda na wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo wamewasili katika mpaka wa Holili wilayani Rombo kufuatia sakata la mahindi kusafirisha kwa njia za magendo.Picha na Janeth Joseph

By Janeth Joseph

Rombo. Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Profesa AdolfMkendana wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo wamewasili katika mpaka wa Holili wilayani Rombo ambapo baadhi ya watu wanadaiwa kusafirisha kwa njia za magendo mahindi kwenda nchini Kenya.

Mawaziri hao wamefika katika huo leo Jumatano Aprili 7, 2021 kushuhudia watu hao wanaosafirisha mahindi kwa kutumia bodaboda baada ya Kenya kuzuia mahindi ya Tanzania kuingia nchini humo kwa madai kuwa yana sumu kuvu.

Aprili 4, 2021 mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira alifanya ziara ya kushtukiza katika mpaka huo na kukuta shehena ya mahindi yakiwa yamepakiwa kwenye magunia eneo la soko la Holili, kwa ajili ya kusafirishwa Kenya.

Kufuatia hali hiyo alimuagiza Kamanda wa polisi mkoani humo, Amon Kakwale kuwachukulia hatua za kinidhamu mkuu wa kituo cha polisi Holili na askari wengine wawili waliokuwa zamu kwa uzembe wa kuruhusu mahindi kupelekwa Kenya kinyume na taratibu. Askari hao tayari wamechukuliwa hatua baada ya kuhamishwa.

Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi


Advertisement
Advertisement