Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe asema Chedema ikishika madaraka, hakutakuwa na ubaguzi wa elimu

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema chama hicho kikishika dola kitabadilisha mfumo wa elimu nchni na kuhakikisha Lugha ya Kiingereza inakuwa lugha ya kufundishia kuanzia madarasa ya awali hadi chuo kikuu.


Hai. Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema chama hicho kikishika dola kitabadilisha mfumo wa elimu nchni na kuhakikisha Lugha ya Kiingereza inakuwa lugha ya kufundishia kuanzia madarasa ya awali hadi chuo kikuu.

Mbowe ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 19, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya ofisi za chama hicho zilizopo Bomang'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Amedai elimu inayotolewa kwa sasa haimjengi mtanzania kuingia katika ushindani wa soko la ajira, kutokana na mfumo wa elimu uliopo kwa sasa.

"Kumekuwa na ubaguzi katika elimu, iko hivi, viongozi wetu wamekuwa wakituhubiria tujifunze kiswahili ni lugha yetu ya Taifa, lakini leo kiswahili hicho kinazungumzwa kwenye shule zetu za kata, viongozi wote na watu wenye uwezo wanasomesha watoto katika shule za mfumo wa kiingereza"

"Chadema tukiingia madarakani, kiingereza ni lugha ya kimataifa, lazima watoto wote wafundishwe na kiingereza kiwe sehemu ya masomo kuanzia chekechea kwa kila mtanzania, hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka".