Mbowe atuhumiwa kwa mauaji ya viongozi wa Serikali

Muktasari:

  • Baada ya kushikiliwa kwa takribani siku mbili, Jeshi la Polisi limesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Baada ya kushikiliwa kwa takribani siku mbili, Jeshi la Polisi limesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe anakabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo za kupanga njama za kufanya vitendo vya kigaidi na kuua viongozi wa Serikali.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime imesema kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa kwamba, Mbowe alikamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza, jambo ambalo si kweli.

“Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika. Hatua hiyo imefikiwa sasa,” alisema Misime.