Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe kuweka alama ya Sh100 milioni kumbukumbu miezi nane gerezani

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza baada ya kutoa sadaka yake ya shukrani leo Jumapili Machi 20, 2022.

Muktasari:

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameweka nadhiri ya kutafuta Sh100 milioni ili kujenga madhabahu katika kanisa la Nshara, Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Hai. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ameweka nadhiri ya kutafuta Sh100 milioni ili kujenga madhabahu katika kanisa la Nshara, Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Mbowe amesema fedha hizo pia zitaweka madirisha na milango katika kanisa hilo, ikiwa ni alama na kumbukumbu ya miezi nane aliyokaa gerezani.

Mbowe ametangaza dadhiri hiyo leo Jumapili Machi 20, 2022 wakati akizungumza baada ya kutoa sadaka yake ya shukrani katika kanisa hilo ambalo ni nyumbani kwao, ambapo amewaomba wote waliomsindikiza kumuunga mkono.

"Kama sehemu yangu ya shukrani nimeweka nadhiri ya kutafuta popote nitakapofanikiwa na ninajua Mungu ataniongoza kuweza kufanikiwa niweze kupata Sh100 milioni, ambayo nitaomba ikajenge madhabahu ya Bwana ikibaki ikajenge madirisha ya nyumba ya bwana na ikibaki ikajenge milango ya kuingia kwenye nyumba ya bwana"

"Hayo maeneo matatu na ukihitaji kupanda mmea uweze kumea ukiwa na afya ni lazima uipande kwenye mbolea na mbolea ya nadhiri hiyo ni ibada ya leo na ndugu zangu mlionisindikiza, tunahitaji kuacha alama ya kudumu, kwamba kila tukija kwenye usharika wetu huu, tukiangalia madhabahu, tunasema miezi nane ya Mbowe gerezani".

"Ningetamani kwenye kazi hii ya Mungu iliyofanyika hapa Nshara, muisaidie familia yangu kuweka kielelezo cha kumbukumbu ya miezi nane niliyoishi gerezani kama tunaamini Mungu ndiye aliyetoa kibali cha mimi kuwa gerezani na kuachiwa huru" amesema Mbowe na kuongeza: "Tupo katika nyumba ya bwana madhabahu ya Mungu nikiiangalia mmefanya kazi kubwa, natamani tumalizie madhabahu hii ya Bwana, pawe mahali pazuri pa kupendeza zaidi pa kumtukuza Mungu"

"Kwa sababu bwana Mungu anatupa baraka nyingi sana na tumtendee nini huyu Mungu... tumtendee nini cha kumshukuru zaidi ya kupiga magoti na kumwambia Mungu tunakwenda kulitengeneza hekalu lako ili na wale wengine wasio wa haki wakapate huduma na waende kuwa watu wa haki". amesema