Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbowe ziarani Afrika Kusini, kuongoza kongamano la DUA

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Picha na mtandao

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumanne ataondoka nchini Tanzania kwenda Afrika ya Kusini kwa ziara ya kikazi ya siku saba.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema, akiwa Afrika ya Kusini, Mbowe kama Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Vyama vya Demokrasia Afrika (DUA) ataongoza kongamano la kwanza la umoja huo litakalodumu kwa siku nne.

Mrema amesema kongamano hilo litahudhuriwa na vyama wananchama wa DUA, viongozi  wa serikali, mabalozi  na wabunge wanaotokana na vyama wanachama wa DUA pamoja na mashirika na taasisi mablimbali za kimataifa.

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo akisaidiana na Waziri Mkuu Mstaafu wa Canada, Stephen Harper anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima wa kongamani litakaloangazia masuala ya uchumi, ulinzi na usalama, demokariasia pamoja na biashara barani Afrika.

Mbowe anatarajiwa kuhitimisha ziara yake Afrika ya Kusini kwa kuongoza kikao cha Bodi ya uongozi ya DUA kitakachofanyika Aprili 30, 2023 kama kilele cha kongamano hili ambalo litahudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika atakayeongoza ujumbe wa chama nchini Afrika ya Kusini.

Mrema amesema, Mbowe akiwa Afrika Kusini atakutana na wafanyabiashara mbalimbali barani Afrika Mei Mosi, 2023 kwa lengo la kujadiliana mikakati mbalimbali ya kisera itakayochochea uondoshwaji wa vikwazo vya ufanyaji wa biashara Afrika ikiwa ni sehemu ya kuwezesha utumiaji wa fursa zitokanazo na eneo huru la kibishara la Afrika “The African Continental Free Trade Area” (AfCFTA).