Mbunge aeleza misiba inavyotumika kumuombea Rais Samia

Saturday August 06 2022
mbunge pic

By Hawa Mathias

Chunya. Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Mbeya (CCM), Suma Fyandomo amemweleza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Wanambeya katika misiba mingi wamekuwa wakitumia kumfanyia maombi kutokana na kazi nzuri anazofanya.

Mbunge Fyandomo amesema leo Jumamosi, Agosti 6, 2022 alipopewa fursa ya kutoa neno katika uzinduzi wa Barabara ya Chunya-Makongorosi yenye urefu wa kilometa 39.

Amesema ameudhuria misiba mingi wakinamama wanapoamka alfajiri kwa ajili ya kufanya maombi, hawaachi kumuombea Rais Samia kutokana na utendaji wake wa kazi uliotukuka.

''Mh Rais wakina mama Mbeya hatuko nyuma kukuombea kwa mambo makubwa unayoyafanya,” amesema

“Umetujengea jengo la kisasa la mama na mtoto katika hosptali ya Rufaa ya Kanda kitengo cha wazazi Meta ambalo mwanamke anapojifungua kwa uchungu mwenza wake anakuwa alimshuhudia,' 'ameesema.

Fyandomo amesema huduma hizo kwa Tanzania hususan kwa Mkoa wa Mbeya zilikuwa bado lakini sasa kwenye hosptali hiyo inaanza kutolewa kwa kuwa na vyumba maalum.

Advertisement

Amesema wanaona namna Rais Samia anavyoupiga mwingi katika kuwaletea maendeleo Watanzania na kwamba wanaunga mkono utendaji wake wa kazi sambamba na kuwaletea mama wa ‘connection’  Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.

Advertisement