Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge aililia Serikali waliothiriwa kwa mvua

Mamia ya wananchi wakiwa wamekwama katika eneo la kwa Msomali wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya kukatika kwa mawasiliano ya barabara kuu ya Moshi-Arusha kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapa.

Muktasari:

  • Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe, ameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), kutoa msaada wa haraka wa kuzinusuru familia za watu takribani 300 wilayani humo zilizoathiriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua ya mawe ya barafu.

Hai. Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe, ameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), kutoa msaada wa haraka wa kuzinusuru familia za watu takribani 300 wilayani humo zilizoathiriwa na upepo mkali ulioambatana na mvua ya mawe ya barafu.

Mvua hiyo iliyonyesha Januari 19, mwaka huu iliwakosesha makazi baadhi ya wananchi katika kijiji cha Lyamungo kati na kitongoji cha Marukeni, wilayani humo baada ya upepo mkali kuangusha miti mikubwa iliyoangukia kwenye makazi ya wananchi na mvua kuharibu ekari zaidi ya 20 za kahawa, migomba ya ndizi na mahindi.

Akizungumzia athari walizokumbana nazo wananchi ha oleo Januari 26 wilayani humo, Mbunge Mafuwe ameiomba Serikali kuona namna ya kuzisaidia familia hizo kwa kuwa mazao waliyotegemea yameteketea.

“Maafa haya yaliyotokea ni makubwa, chakula tunachokitegemea ni cha ndizi zao tunalotegemea la kutupatia kipato na kula. Ukitizama kahawa nayo imeharibiwa, karibu wananchi 300 kahawa zimeondoka na migomba imeondoka.

"Namwomba Waziri Jenista Mhagama ambaye yupo Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, uje uone hili, kwa sasa maeneo haya hatuna chakula, tunaomba sana Rais wetu Samia Suluhu Hassan tunafahamu namna ambavyo unatupenda wananchi wako," amesema.

Aliongeza "Ninafahamu Mkuu wa wilaya pamoja na kamati yake ya maafa ya wilaya anaendelea na tathmini ya wilaya ili iweze kuletwa rasmi, lakini naomba Serikali itakavyoona inafaa kwa uharaka itusaidie maana watu hawana chakula ili tuweze kuondokana na ukiwa huu ambao umetufika.”

Mwananchi wa kitongoji cha Marukeni, Josephine Mushi, ameishukuru Serikali kwa namna walivyofika kwa haraka katika maeneo hayo kuona athari za mvua hizo.

"Tunaishukuru Serikali kwa namna ambavyo ilitukimbilia wakati tulipokutwa na changamoto hii, tumefarikijika kumwona mbunge kuja kutukimbilia katika maafa haya maana yalikuwa ni makubwa," amesema.

Naye Fredrick Shuma amesema: "Tumepata hasara kubwa sana, ni njaa ambayo hatutakaa tuisahau, maana tukio hili ni la mara ya kwanza kutokea katika kitongoji hiki na ni kama kitongoji chote kizima kimepata majanga haya."

Januari 21, Mkuu wa Wilaya hiyo, Amir Mkalipa alisema tayari Serikali imeanza kufanya tathmini ya maeneo yaliyoathiriwa na mvua hizo ili kuona ni namna gani ya kuwasaidia wananchi hao.