Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge asimulia ajali iliyomkuta

Muktasari:

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Machi 30 baada ya gari kupinduka lakini hakuna aliyeumia licha ya gari kuharibika

Iringa. Mbunge wa Mafinga Mjini (CCM), Cosato Chumi ameeleza jinsi alivyopata ajali akiwa na familia yake katika eneo la njia panda ya Tosamaganga wilayani Mafinga mkoani Iringa usiku wa kuamkia jana Machi 30, 2018.

Ajali hiyo ilitokea karibu muda sawa na ajali iliyowapata wabunge wengine sita wa Zanzibar waliokuwa wakitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam, ambao walipata  ajali eneo la Bwawani, Morogoro.

Akizungumza leo Jumamosi Machi 31, 2018 Chumi amesema ajali hiyo ilitokea alipofika katika njia panda ya Tosamaganga kilometa 20 kutoka Iringa Mjini baada ya gari kuserereka na kupinduka.

“Nilikuwa na mke na watoto wangu nawapeleka kwa bibi yao kwa ajili ya kula Sikukuu ya Pasaka. Tulipofika njia panda ya Tosamaganga gari ilipinduka, lakini nashukuru hakuna aliyeumia, japo gari limeharibika vibaya,” amesema Chumi.