Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbunge awataka wananchi kulima kilimo cha umwagiliaji

Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe  akizungumza na wananchi wa kata ya Narumu.

Muktasari:

Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kulima kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika ambapo Serikali imetoa Sh500 milioni kwa ajili ya kilimo hicho.

Hai. Mbunge wa Hai, Saashisha Mafuwe amewataka wananchi wa Wilaya hiyo kulima kilimo cha umwagiliaji ambacho ni cha uhakika ambapo Serikali imetoa Sh500 milioni kwa ajili ya kilimo hicho.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Narumu, Mafuwe amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kukarabati vyanzo vya maji kwa ajili ya umwagiliaji pamoja na kuzibua mifereji ambayo iliharibiwa na mafuriko mwaka jana.

"Wizara ya Kilimo imetoa Sh300 milioni kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na tunasubiri nyingine Sh200 milioni, fedha hizi zitatumika kukarabati vyanzo vya maji ya umwagiliaji vilivyoharibiwa na mafuriko ikiwemo chanzo cha maji cha Makeresho,"amesema Mbunge Mafuwe

"Najua wananchi mmepata changamoto nyingi kutokana na mafuriko ya mwaka jana ambayo yalipelekea vyanzo vyetu vya maji na mifereji ya umwagiliaji kuziba na kuwapelekea wakulima kukosa maji ya kunyeshea mazao yenu,serikali yetu imeliona hilo ndio maana imetoa Sh500 milioni kuondoa changamoto iliyojitokeza" amesema

Amewataka wananchi kuhakikisha wanatumia maji hayo vizuri kulima kilimo cha kahawa, migomba na vanila ambayo yamekuwa ni mazao yanayokuza uchumi katika Jimbo hilo.

"Maji haya yakishapatikana nikahakikisha kila kaya ina maji kwa kweli tutalazimishana kulima zao la kahawa,vanila na migomba  maana uchumi wetu mkubwa na uliotufikisha hapa tulipo ni kahawa,"amesema Mafuwe

Wakizungumza katika mkutano huo, wananchi wa Kata ya Narumu wameipongeza Serikali kwa kutenga fedha hizo kwa ajili ya kilimo ambapo wamesema kilimo cha umwagiliaji kimekuwa ni mkombozi wa wananchi  wengi kwani kimekuwa ni kilimo chenye manufaa makubwa.