Mbunge CCM afariki dunia

Mbunge Umbulla afariki dunia

Muktasari:

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara,  Martha Umbulla amefariki dunia jana Jumatano Januari 20, 2021  katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.  

Dar es Salaam. Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara,  Martha Umbulla amefariki dunia jana Jumatano Januari 20, 2021  katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.  

Kifo cha mbunge huyo aliyezaliwa Novemba 10, 1955 kimetangazwa leo Alhamisi Januari 21, 2021 na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

 “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.”

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina,” amesema Ndugai.