Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Meya Kigoma Ujiji afunguka kuhusu safari ya Marekani

Meya wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, Hussein Ruhava (aliyesimama) akizungumza kwenye mkutano na wananchi. Picha ya Maktaba.

Muktasari:

  • Ruhava ambaye aliingozana na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP), amesema  kuwa mkutano huo utaleta maarifa mapya, kupanua fursa za biashara, mitaji mipya kutoka nje ya nchi na kutanua utalii wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla.

Dar es Salaam. Meya wa Manispaa ya Kigoma-Ujiji, Hussein Ruhava (ACT-Wazalendo) amesema safari yake ya kikazi aliyofanya nchi Marekani imefungua milango ya fursa mbalimbali kwa manispaa yake na Taifa kwa ujumla.

Ruhava ambaye aliingozana na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe nchini humo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa siku mbili wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP), amesema  kuwa mkutano huo utaleta maarifa mapya, kupanua fursa za biashara, mitaji mipya kutoka nje ya nchi na kutanua utalii wa Kigoma na Tanzania kwa ujumla. 

Pia, Meya huyo amesema  Kigoma- Ujiji ambayo ilikuwa miongoni mwa manispaa 15 zilizopata nafasi ya kushiriki mkutano huo, imeazimia  kutumia maarifa hayo kuweka  mpango mkakati wa kusimamia na kuboresha sekta ya afya, maji, elimu, ardhi, uwazi katika bajeti na uwazi katika takwimu.