Meya Ujerumani asimamishwa kwa kuwahi chanjo ya corona

Thursday April 08 2021
MEYAUJERUMANIPIC

Berlin, Ujerumani (AFP). Meya mmoja nchini Ujerumani amesimamishwa na baraza lake la jiji baada ya kubainika kuwa alipata chanjo ya virusi vya corona mwezi Januari, licha ya kutokuwa katika kundi la waliopewa kipaumbele cha kuchanjwa kwanza.

Madiwani wote 34 waliopiga kura jana Jumatano, waliazimia kumsimamisha kwa muda meya huyo wa jiji la Halle anayeitwa Bernd Wiegand.

Awali Wiegand, 64, alikubali kuwa alipata chanjo hiyo mwezi Januari, kipindi ambacho ilikuwa ikitolewa kwa wazee tu.

Wafanyakazi wengine wa jiji hilo na madiwani kadhaa waliripotiwa kupata chanjo hiyo kabla ya zamu yao.

Meya huyo alikana kuwa alipata chanjo hiyo isivyo halali na kwamba hakufuata maadili, hata hivyo alisema alipewa chanjo ili kuepuka dozi za ziada kutuopwa.

"Ni rahisi kukosoa uamuzi wangu... lakini haukuwa wa kukiuka sheria kwa njia yoyote," alisema katika taarifa aliyioitoa m,wezi Machi, akimaanisha kuwa kashfa hiyo imeibuliwa ili kumuondoa ofisini meya ambaye hana chama.

Advertisement
Advertisement