Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mfanyabiashara aliyevamiwa, kujeruhiwa Njombe afariki dunia

Duka la mfanyabiashara, Godfrey Ndambo likiwa limefungwa, ambapo hapo ni moja ya sehemu ambayo alikuwa anafanya biashara zake enzi za uhai wake. Picha na Seif Jumanne

Muktasari:

  • Kamanda wa Polisi, Mahamoud Banga, ametaka wafanyabiashara wawe na CCTV na kuhifadhi fedha salama, huku Sifaely Msigala akiomba usalama zaidi.

Njombe. Mfanyabiashara maarufu katika mji wa Njombe, Godfrey Ndambo (45) aliyevamiwa na majambazi maeneo ya nyumbani kwake wakati akitokea kwenye biashara zake na kupigwa na kitu kizito kichwani kilichosababisha majeraha, amefariki dunia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Julai 22, 2024 amesema tukio hilo lilitokea Julai 20, 2024, saa 2:30 usiku katika eneo la Uzunguni, Kata ya Ramadhani, Halmashauri ya mji wa Njombe.

Banga amesema wahusika wa tukio hilo ambao idadi yao haijafahamika, walimpiga mfanyabiashara huyo na kutoweka na fedha zinazokadiriwa kuwa ni Sh47 milioni.

"Baada ya kujeruhiwa alitibiwa katika Hospitali ya Kibena na baadaye alihamishiwa mkoani Mbeya wakati matibabu yakiendelea akafariki dunia," amesema Banga.

Amesema jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi wa kina na baadaye watatoa taarifa ya watu watakaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Kamanda huyo amewataka wafanyabiashara mkoani Njombe kufunga kamera maeneo wanayoishi na ziwe wazi muda wote, kwani linapotokea tukio ni rahisi kwa polisi kuanza kufanya uchunguzi kupitia kamera hizo.

"Changamoto tuliyoipata pale kwa marehemu kuna CCTV kamera, lakini haikuwa inafanya kazi, kwa hiyo mara nyingi alipokuwa anarudi nyumbani ndiyo alikuwa anaiwasha " ameongeza Banga.

Pia amewataka wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa wahakikishe hawalali na fedha nyingi nyumbani, kwani zipo taasisi za fedha ambazo kupitia mashine za kutolea fedha (ATM) wanaweza kuweka fedha zao hata usiku.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara Nyanda za Juu Kusini, Sifaely Msigala ameiomba Serikali kuongeza jitihada ili kuona namna gani wataishi kwa amani kwa sababu wanajipanga kuona namna gani tutaongeza muda wa kufanya biashara.

Mmoja ya wafanyabiashara mkoani Njombe, Petro Migoha amesema ukosefu wa elimu ya kutosha kuhusu kutembea na fedha nyingi bila kuwa na ulinzi unachangia matukio ya aina hiyo.