Mifumo ya maisha, lishe duni inavyoleta madhara

Lishe na joto vyatajwa chanzo cha ugumba

Muktasari:

Mtindo wa maisha ya watu katika miji mbalimbali wa kutozingatia lishe bora na mapumziko, umetajwa kutishia mfumo wa afya za wakazi wa maeneo hayo.

Dar es Salaam. Mtindo wa maisha ya watu katika miji mbalimbali wa kutozingatia lishe bora na mapumziko, umetajwa kutishia mfumo wa afya za wakazi wa maeneo hayo.

Hata hivyo, hatua za kimkakati za kukabiliana na tishio hilo zinatakiwa kuchukuliwa, watafiti nchini wamebainisha.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na madaktari wa moyo Dar es Salaam ukiwahusisha zaidi ya watu 6,000 wenye umri kati ya miaka 20 hadi 70, umegundua kuwa tabia hizo hatari za lishe zimechagizwa na gharama ya chakula.

“Bei ya soda ya sasa ni sawa na ile ya maji ya kunywa ya chupa na chakula cha haraka kama chipsi ni rahisi kuliko chakula chenye afya kinachotengenezwa hapa nchini,” unasema utafiti huo.

Habari kamili jipatie nakala yako ya Mwananchi leo Alhamisi Machi 04, 2021