Miili 19 ya waliofarika ajali ya ndege yawasili Kaitaba

Majeneza yenye miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Jumapili Novemba 6, 2022 ikiwa imebeba watu 43 kutumbukia katika Ziwa Victoria, Bukoba mkoani Kagera.

Muktasari:

Miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege Bukoba tayari imewasili uwanja wa Kaitaba kwa ajili ya ibada na heshima za mwisho kabla kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.

Bukoba. Miili ya watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege Bukoba tayari imewasili uwanja wa Kaitaba kwa ajili ya ibada na heshima za mwisho kabla kukabidhiwa kwa ndugu kwa mazishi.


Ibada hiyo inatarajiwa kuongozwa na viongozi wa dini na madhebu mbalimbali ambao tayari nao wamefika uwanjani hapo.


Miongoni mwa viongozi wa dini waliofika uwanja wa Kaitaba ni Kaimu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Method Kilaini, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kazikazini Magharibi, Abednego Kashomshahara.


Wengine ni Shekh wa Mkoa wa Kagera, Hatuna Kichwabuta na kiongozi wa Kanisa la Adonai Internation King James.


Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila, maandalizi yote ya ibada kitaifa na heshima za mwisho kwa marehemu hao yamekalika kabla miili hiyo kukabidhiwa kwa ndugu kwa taratibu na mazishi ya kifamilia.