Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mipaka ya Holili, Horohoro yapigwa jeki ujenzi wa vyoo

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Shirika la WaterAid kwa kushirikiana na Mtandao wa asasi zisizo za serikali zinazojihusisha na masuala ya maji na usafi wa mazingira (TAWASA NET) wamekabidhi mradi wa vyoo vya kisasa  vyenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni katika mipaka  ya Holili na Horohoro.

Rombo. Shirika la WaterAid kwa kushirikiana na Mtandao wa asasi zisizo za Serikali zinazojihusisha na masuala ya maji na usafi wa mazingira (TAWASA NET) wamekabidhi mradi wa vyoo vya kisasa vyenye thamani ya zaidi ya Sh100 milioni katika mipaka ya Holili na Horohoro.

 Akizungumza wakati akikabidhi mradi wa choo katika mpaka wa Holili uliopo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Mhandisi wa Shirika la WaterAid nchini, Gloria Kafuria amesema mradi huo wa Holili utasaidia kuhudumia wananchi 1500 kwa siku wanaopita katika mpaka huo ili  kusaidia  kukabiliana na ugonjwa wa uviko 19 pamoja na utunzaji wa mazingira.

"Sisi kama Water Aid Tanzania tumeweza kukamilisha mradi huu wa vyoo hapa mpaka wa Holili, mradi huu ni sehemu ya miradi ambayo tumefanya hapa nchini kwa ajili ya kutoa huduma za vyoo katika maeneo ya mipakani hasa katika kukabiliana na uviko 19 kwenye haya maeneo,"

"Mradi huu wa Holili umegharimu Sh43 milioni na Mradi wa Horohoro umegharimu Sh67milioni lengo ni kuweza kuwasaidia wananchi wanaopita katika maeneo haya ya mipaka yetu,mradi huu wa vyoo hivi hapa mpakani utaweza kuwahudumia watu zaidi ya 1500 kwa siku,"

Naye Mwenyekiti wa TAWASA NET, Mhandisi Herbert Kashilila amesema mtandao huo umekuwa ukishirikiana na jamii kupunguza athari za magonjwa yanayotokana na maji, usafi wa mwili katika maeneo ya mipakani hasa katika kipindi hiki cha Uviko-19.

"Kwa Kushirikiana na WaterAid Afrika Mashariki mwanzoni tuliweka kituo cha kunawa mikono ili kupunguza maambikizi kutoka upande mmoja kuingia upande mwingine na leo hii tumekabidhi vyoo hivi vya kisasa ili kwenye eneo hili la mpaka liweze kuwa na usafi zaidi,"amesema Kashilila.

Ofisa Afya Mfawidhi Mpaka wa Holili,Kassele Koba amesema licha ya kukabidhiwa vyoo hivyo vya kisasa eneo hilo la mpaka wa Holili linakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maji na kuwaomba wadau hao kuangalia namna ya kuwawekea miundo mbinu ya maji ili kuweza kuvihudumia vyoo hivyo.