Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mitaala iliyopitwa na wakati kufutwa SUA

Muktasari:

  • Mafunzo hayo yamelenga kujengewa uwezo wa kukuza mitaala ikiwa ni mchakato wa uboreshaji wa mitaala ukilenga wanafunzi kupata maarifa na fursa za kujenga ubunifu huku sababu ikitajwa mitaala iliyopo baadhi yake imepitwa na wakati.

Morogoro. Ili kuendana na kasi ya teknolojia duniani, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro kinatarajia kuanza kufumua mifumo ya mitaala ya taaluma kufuatia baadhi ya mitaala kupitwa na wakati mkoani Morogoro.

 Hatua hiyo inakuja baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku tatu ya mchakato wa kuwajengea uwezo wa uborejeshaji wa mitaala washiriki ambao ni wakuu wa idara mbalimbali katika chuo hicho mkoani hapa.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo mkoani hapa, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalamu Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro, Profesa Maulid Mwatawala amesema wanalenga kufuta, kuboresha na kuingiza mitaala mipya baada ya iliyopo baadhi yake kupitwa na wakati.

Profesa Mwatawala amesema mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga kuwajengea uwezo wakuu wa idara mbalimbali ili kuwawezesha kuwa na uwezo zaidi wa kuandaa mitaala mipya, kuboresha baada ya mitaala mingine kufutwa kwa kupitwa na wakati.

“Tumeanza mafunzo kuhusu maboresho ya mitaala ambayo ni sehemu ya mradi wa elimu ya juu  kwa maboresho ya mabadiliko  ya uchumi Tanzania (Hit) katika kuboresha kuingiza masuala ya stadi. Pia soko la ajira na matakwa ya soko la ajira na kupitia mitaala iliyopitwa na wakati na ipo itayoboreshwa ili kuingia katika mapinduzi ya viwanda na kuingia katika uchumi wa viwanda ikiwa ni maboreshio ya kawaida ya kupitia maboresho,”amesema Profesha Mwatawala.

Kaimu Rasi Ndaki ya Misitu, Wanyamapori na Utalii Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Morogoro, Dk Agnes Sirima amesema uwepo wa mafunzo hayo yataleta tija kwao na kupata mwanga katika kuandaa mitaala hiyo ili kuendana na matakwa ya sasa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Uboreshaji wa Mitaala Chuo Kikuu cha Kilimo ch Sokoine (Sua), Dk Jamal Athuman mafunzo hayo yanashirikisha marasi wa ndani, maamidi wa shule, wakuu wa idara za taaluma, wenyeviti wa kamati za wakuza mitaala na kamati za wakuu wa mitaala ya chuo hicho.