Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke afia kwenye gesti ya mumewe

Nyumba ya kulala wageni (gest)ambayo Mwanamke aliyetambulika kwa jina la Naomi anadaiwa kujinyonga kwenye choo cha nyumba hiyo.

Muktasari:

  • Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa mji mdogo Katoro wilayani Geita mkoani hapa amekutwa amejinyonga kwa kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na mumewe.

Geita. Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Naomi mkazi wa mji mdogo Katoro wilayani Geita mkoani hapa amekutwa amejinyonga kwa kamba ya manila ndani ya choo cha nyumba ya kulala wageni inayomilikiwa na mumewe.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Henry Mwaibambe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho.

Tukio hilo limetokea Februari 3, 2022 saa 12 jioni baada ya mwanamke huyo kufika kwenye nyumba ya wageni na kumtaka mmoja wa wahudumu amsaidie mtoto mwenye umri wa miezi minne kwa kuwa yeye anajisikia vibaya.

Akizungumzia tukio hilo, mhudumu wa nyumba hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Monica Paul amesema, mke wa mwajiri wake alifika kwenye eneo hilo saa 8 mchana na kumtaka amsaidie mtoto ili yeye apumzikekwa kuwa hayuko vizuri kiafya.

Amesema baada ya hapo alipewa chumba, lakini baadaye walikuta mwili ukining’inia juu chooni, baada ya mteja mwingine kuomba huduma ya choo alichojinyongea mwanamke huyo.

Kiongozi wa eneo hilo, Stephano Bandola amesema hawajajua chanzo cha mwanamke huyo kujinyonga lakini akadai inaweza kuwa mgogoro wa kifamilia.

Juhudi za kumpata mume wa mwanamke huyo hazikufanikiwa baada ya kuelezwa yuko safarini nje ya Katoro.