Mke wa Bush afariki dunia
Muktasari:
Mwanawe aliongoza Marekani mwaka 2000
Washington, Marekani. Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92.
Ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa Taifa hilo, George HW Bush ambaye ni mumewe na mwanawe George W Bush.
Barbara aliyekuwa mke wa rais mwaka 1989 hadi 1993 aalikuwa mgonjwa kwa kwa muda mrefu na alikataa kupatiwa matibabu.
Rambirambi zimekuwa zikitumwa nchini Marekani kutoka maeneo mbalimbali duniani.
Mumewe George HW Bush ana miaka 93.
Mtoto wake George W Bush aliingia madarakani mwaka 2000 na kuongoza mihula miwili akiwa Rais wa 43 wa Marekani.
"Mama yangu mpendwa ametuacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura, Barbara, Jenna nami tunaomboleza lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika," amesema George W Bush katika rambirambi zake.