Mke wa Dk Mwaka adai hajapewa talaka, itamfuata alipo

Muktasari:

  • Sakata la ndoa ya Dk Juma Mwaka bado kizungumkuti baada ya mkewe Queen Masanja kudai hadi sasa bado hajapewa talaka.

Dar es Salaam. Sakata la ndoa ya Dk Juma Mwaka bado kizungumkuti baada ya mkewe Queen Masanja kudai hadi sasa bado hajapewa talaka.

Sakata hilo lilichukuwa sura mpya baada ya kikao cha Kamati ya Masheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa aliyekuwa sheikh wa mkoa, Alhadi Mussa Salum kuketi kwa dharura na kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka.

Hata hivyo, uamuzi huo ulipingwa na Baraza la Ulamaa Januari 27, 2023 ikieleza uamuzi huo ni batili.

Akizungumza leo Machi 20, 2023 jijini Dar es Salaam Queen wakati akitangazwa kuwa balozi wa kampuni inayojishughulisha na uuzaji na uagizaji wa magari ya BM amesema kuwa hadi sasa bado hajapewa huku akieleza kuwa mchakato wake unaendelea.

“Kwa upande wa talaka, bado sijapata talaka lakini ipo katika mchakato na ninaamini itanifata niliko”alisema.

Pia ametoa wito kwa wanawake kupambana kujitafutia maendeleo licha changamoto mbalimbali za kifamilia  na kijamii  wanazopitia. Amesema baadhi ya wanawake wanapitia magumu katika familia lakini  amewataka kutokata tamaa.

"Mimi ni mama, natambua mchango wa mwanamke katika familia na ili kuwa mama bora lazima upambane  kwa ajili ya familia yako kwa kufanya kazi kwa bidii"