Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mmoja auawa vurugu za wafanyakazi na Askari

Mwili wa mfanyakazi wa kiwanda cha Sukari Mkulazi kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro Nawabu Almas ukiwa chini baada ya kudaiwa kupigwa risasi na askari wa Shima. Lilian Lucas

Muktasari:

  • Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema chanzo cha mauaji hayo ni kutoelewana kati ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi na Askari wa Kikosi cha Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza.

Morogoro. Vurugu kati ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi na Askari wa Kikosi cha Shirika la Uzalishaji Mali Jeshi la Magereza (Shima), zinadaiwa kuondoa uhai wa kijana mmoja, Nawabu Almas (36), aliyekuwa mfanyakazi katika kiwanda hicho.

Kifo cha Nawabu kinadaiwa kutokea leo Jumanne Oktoba 17, 2023 saa 12:00 asubuhi akidaiwa kupigwa risasi wakati wa vurugu hizo.

Akizungumza katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema chanzo cha mauaji hayo ni kutoelewana kati ya askari hao na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

“Taarifa nilizozipata ni kuwa baadhi ya wafanyakazi wanaingia na mabegi na wanatoka na baadhi ya vifaa vya ujenzi wa mradi huo wa kiwanda na ndio chanzo cha ugomvi na vurugu kutokana na kuzuiwa kuingia na chochote kiwandani," amesema.

Kutokana na kifo cha Nawabu, Malima amewasihi wafanyakazi wa kiwanda hicho kuwa watulivu wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea kufanyika.

Baada ya tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka alifika katika eneo hilo pamoja na vikosi vya ulinzi na usalama kutuliza ghasia.

Kulingana na taarifa ambazo Mwananchi Digital imezipata, mwili wa marehemu huyo awali ulihifadhiwa katika hopsitali ya St Joseph Dumila na mipango ya kuuhamishia katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya uchunguzi zaidi inaendelea.

Kiongozi wa wafanyakazi, Henry Sengira amesema mara kadhaa kumekuwa na hali ya kutokuelewana kati ya pande hizo mbili, huku askari hao wakitumia lugha zisizo za staha.

“Nakuomba mkuu wa mkoa jambo hili lishughulikie kwa karibu na haraka ili madhara zaidi yasiendelee kutokea,” amesema Sengira.