Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wateketeza mabweni matatu Kilimanjaro

Mabweni matatu ya wasichana katika shule ya sekondari Nyerere iliyopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro yameteketea kwa moto. Picha na Janeth Joseph

Muktasari:

Moto huo ambao umezuka leo Septemba 14, 2022 umeunguza mabweni matatu ya wasichana ambapo wanafunzi zaidi ya 100 watalazimika kulala madarasani, huku serikali ikiangalia utaratibu wa kukarabati mabweni hayo.

Mwanga. Wanafunzi zaidi ya 100 katika shule ya sekondari Nyerere iliyopo Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro watalazimika kulala madarasani baada ya mabweni yao kuteketea kwa moto ambao chanzo chake hakijajulikana bado.

Kufuatia kutokea kwa ajili hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameuagiza uongozi wa wilaya ya Mwanga kuchunguza chanzo chake.

Babu ametoa maagizo hayo leo Septemba 14, 2022 wakati alipotembelea shule hiyo kuangalia athari za moto huo ambao umeteketeza madaftari ya wanafunzi, magodoro, mablanketi pamoja na vitu mbalimbali vilivyokuwa mabwenini.

"Tunamshukuru Mungu wakati moto unatokea wanafunzi hawakuwa mabwenini. Kwa sasa serikali tunaangalia namna ya kuwasaidia wanafunzi hawa kwa sasa,"

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Nyerere iliyopo wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wakichambua baadhi ya madaftari kwenye mabaki ya masalia ya moto ambao umeteketeza mabweni matatu. Picha na Janeth Joseph

"Lakini nimeambiwa moto huu leo ni mara ya nne unatokea kwenye hii shule. Uliotokea mwaka jana umetokea tarehe sawa na ya leo na mwezi kama huu huu wa leo," amesema.

"Nauagiza uongozi wa Wilaya hii ya Mwanga kuchunguza majanga haya ya moto katika shule hii ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara ili tujue hasaa chanzo cha moto huu unatokana na nini," amesema RC Babu.