Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Moto wateketeza Soko la Mashine Tatu Iringa, uchunguzi waendelea

Muonekano wa Soko la Mashine Tatu lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa likiwa linaungua usiku wa kuamkia leo Julai 12, 2025.

Muktasari:

  • Soko la Mashine Tatu, Iringa limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia Julai 12, 2025 huku maduka na vibanda kadhaa vimeungua na chanzo cha moto bado kikichunguzwa.

‎Iringa. Soko maarufu la Mashine Tatu lililopo katika Manispaa ya Iringa limeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo Julai 12, 2025, ambapo vibanda na maduka kadhaa vimeteketea huku chanzo cha moto huo kikiwa bado hakijafahamika.

‎Mwananchi Digital ilifika katika eneo hilo alfajiri ya leo Jumamosi Julai 12, 2025 na kushuhudia moto ukiendelea kuwaka huku baadhi ya wafanyabiashara wa eneo hilo wakikusanyika kuangalia mali zao zikiendelea kuteketea.

‎Baadhi yao wamesema walipokea taarifa za moto saa nane usiku lakini juhudi za kuuzima zilikuwa ngumu kutokana na kuchelewa kuukabili.

‎Mamlaka husika za usalama zikiwemo Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto tayari wapo eneo la tukio kwa uchunguzi wa awali huku wakiwahimiza wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati taratibu za kubaini chanzo cha moto huo zikiendelea.

‎Kwa taarifa zaidi, endelea kufuatilia Mwananchi na mitandao yetu ya kijamii.