Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mradi wa kupinga ukatili kwa wenye ulemavu waiva

Mkuu wa Miradi wa shirika la C-Sema, Michael Marwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mradi wa miaka mitatu kwaajili ya kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto wenye ulamavu wilayani Butiama. Picha na Beldina Nyakeke

Muktasari:

Shirika lisilokuwa la kiserikali linaloshughulika na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa watoto la C- Sema linatarajia kutekeleza mradi wa miaka mitatu wa kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto wenye ulemavu Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Butiama. Shirika lisilokuwa la kiserikali linaloshughulika na mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwa watoto la C- Sema linatarajia kutekeleza mradi wa miaka mitatu wa kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto wenye ulemavu Wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Mkuu wa Miradi wa shirika hilo, Michael Marwa amewaambia waandishi wa habari leo Jumapili Agosti 6, 2023 mjini hapa kuwa  mradi huo ujulikanao kama Chaguo langu Haki yangu unalenga kuwapa nafasi watoto wenye ulemavu kupata haki zao kama watoto wengine.

Amesema katika utafiti waliofanya wamebaini kuwa watoto wengi wenye ulamavu wanafanyiwa ukatili lakini wanashindwa kupata msaada kama ilivyo kwa watoto wengine.

“Huu mradi unalenga kulinda haki na kuwapa nafasi mabinti na wanawake hasa wenye ulamavu kuwa huru kwasababu tumebaini ukatili kwa watu hawa ni mkubwa zaidi kuliko kwa makundi mengine,

"Sina takwimu kwa sasa lakini mahitaji ya mradi kama huu kwa hapa Butiama na Mkoa wa Mara ni makubwa kama mnavyojua mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa ya  vitendo vya ukatili kwa watoto sasa kwa watoto wenye ulemavu hali ni mbaya zaidi kwasababu hawana namna ya kujipambania,"amesema Marwa

Amesema kundi hilo linashindwa kupigania haki zao kutokana na hali zao hivyo jitihada kutoka  kwa wadau zinahitajika ili waweze kuwa huru na kuondokana na vitendo hivyo.

Ofisa Maendeleo Msaidizi Wilaya ya Butiama, Aminani Mfinanga amesema licha ya  vitendo vya ukatili kwa watoto wenye ulemavu kuwa vingi wilayani humo lakini jamii bado haijawa tayari kushirikiana na Serikali katika kuvitokomeza.

Amesema mara nyingi wanapopata taarifa juu ya uwepo wa vitendo hivyo jamii haipo tayari kutoa  ushirikiano hivyo kesi nyingi huishia polisi badala ya mahakamani kama inavyotakiwa, akiwataka wakazi wa wilaya hiyo kuungana kupiga vita vitendo hivyo kwakuwa watu wenye ulemavu nao wana haki sawa na watu wengine.

"Kwa mwaka huu tuna kesi mbili ambapo moja tayari imetolewa hukumu na nyingine bado inaendelea  mahakamani lakini sio kwamba vitendo havipo, vipo vingi shida ni ushirikiano ili tuweze kupata ushahidi wa kupeleka mahakamni kwa hatua zaidi," amesema Aminani

Ofisa Madini ya Jamii Wilaya ya Butiama, Atula Sanga amesema watoto wenye ulemavu wanapitia changamoto nyingi za ukatili wa kijinsia kulingana na hali zao.

"Kundi hili linafanyiwa ukatili mkubwa zaidi kuliko makundi mengine, hawana sehemu nzuri za kulala, lishe duni, wanabakwa na hata kuitwa majina yasiyofaa," amefafanua