Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mshindi wa kwanza wa mashindano ya Qur'an 2024, afariki dunia

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti mbalimbali za habari nchini humo zinaeleza kuwa Sow alifariki, baada ya kuugua ghafla ingawa familia haijatoa maelezo rasmi kuhusu chanzo kamili cha kifo chake.

Abidjan. Mshindi wa mashindano ya Kimataifa ya Quran Tukufu 2024 Ibrahim Sow (17) raia wa Ivory Coast ameripotiwa kufariki dunia Jumanne Julai 15, 2025 nchini Ivory Coast.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka tovuti mbalimbali za habari nchini humo zinaeleza kuwa Sow alifariki, baada ya kuugua ghafla ingawa familia haijatoa maelezo rasmi kuhusu chanzo kamili cha kifo chake.

Sow alijizolea umaarufu mkubwa mwaka 2024 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’an yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Ushindi huo ulimuwezesha kushinda Sh27 milioni ambazo alikabidhiwa na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi.

Umahiri wake katika kuhifadhi na usomaji wa Qur’an tukufu vilimpa heshima na umaarufu si tu barani Afrika bali pia katika jumuiya mbalimbali za Waislamu duniani.

Baada ya kutangazwa kwa kifo chake kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, watu kutoka mataifa mbalimbali wametoa salamu zapole huku wakieleza namna alivyokuwa mfano wa kuigwa kwa vijana.