Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtandao wa bure kupatikana nyumbani kwa Lowassa

Maandalizi mbalimbali yakiendelea  nyumbani kwa Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa, katika kijiji cha Ngarash,Monduli leo Alhamisi Februari 15,2024. Picha na Janeth Mushi

Muktasari:

  • Shirika la Simu Tanzania (TTCL) limeweka mtandao utakaowezesha waombolezaji watakaofika msibani nyumbani kwa Edward Lowassa kutumia bure mtandao wa intaneti.

Monduli. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa huduma ya bure ya mawasiliano ya mtandao wa intaneti katika makazi ya Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hiyo.

 Huduma hiyo imeunganishwa kuanzia jana Jumatano Februari 14, 2024 nyumbani hapo katika Kijiji cha Ngarash wilayani Monduli.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk Jabir Bakari ameeleza ili kufanikisha shughuli ya mawasiliano kwa waombolezaji nyumbani hapo, Shirika la Simu Tanzania (TTCL) limeweka mtandao utakaowezesha waombolezaji watakaofika msibani kutumia bure mtandao wa intaneti.

"Ili kuhakikisha mawasiliano yanapatikana vizuri, kama ambavyo mnafahamu eneo hili ni miongoni ambalo lina  mawasiliano ya kawaida ya mitandao yote ila kwa sababu litakuwa na watu wengi kwa ghafla ilibidi juhudi za ziada zifanyike kwa maana watoa huduma wa ‘adjust’ kidogo mitambo yao ili watu wengi watakapokuwa hapa wapate huduma na TTCL wametoa mtandao wa bure wa intaneti," amesema.

Katika hatua nyingine, leo Alhamisi Februari 15, 2024 maandalizi yanaendelea kijijini hapo.

Baadaye mchana mwili wa Lowassa unatarajiwa kuwasili ukitokea jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa wilaya na mkoa wameanza kuwasili nyumbani hapo, ambako kesho Februari 16, 2024 mwili wa Lowassa utaagwa kabla ya maziko yatakayofanyika Jumamosi Februari 17, yakitarajiwa kuhudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.