Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto aliyedaiwa kufa kwa njaa afukuliwa, azikwa

Muktasari:

  • Mtoto Salah Jackson (5) aliyezikwa na mama yake kimyakimya usiku baada ya kudaiwa kufa njaa, leo amezikwa rasmi katika kijiji cha Makiwaru wilayani hapa Mkoa wa Kilimanjaro.


Siha. Mtoto Salah Jackson (5) aliyezikwa na mama yake kimyakimya usiku baada ya kudaiwa kufa njaa, leo amezikwa rasmi katika kijiji cha Makiwaru wilayani hapa Mkoa wa Kilimanjaro.

Mtoto huyo alifariki dunia Aprili 21 na kisha mama yake aitwaye Rebecca Siowi (30) kumzika kimya kimya katika nyumba ya mama yake baada ya mume wake kumtelekeza akiwa na watoto watano.

Kutokana na tukio hilo la mama kumzika mwanaye mwenyewe usiku wa manane liliwaibua Jeshi la polisi mkoani hapa ambapo mwili wa mtoto huyo ulifukuliwa Aprili 22, kwa ajili ya kwenda kuufanyia uchunguzi wa kina kujua uhalali wa kifo cha mtoto huyo.

Hata hivyo, alipotafutwa Kamanda wa polisi Mkoani hapa, Simon Maigwa alisema baada ya kuufukua mwili wa mtoto huyo ulipelekwa hospitali kwa ajili ya kuufanyia uchunguzi ambapo mtoto huyo alibainika kuwa alikufa kwa njaa kwa mujibu wa majibu ya madaktari.