Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mvua yaharibu barabara, madaraja Mbinga

Mbinga. Serikali imeidhinisha kiasi cha Sh672 milioni kwa ajili ya kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara na madaraja ya vijiji vinne vya Mapera, Mikaranga, Ilela na  Mitawa ambayo imeharibiwa vibaya na  mvua na kusababisha mawasiliano kukatika.

Akizungumza na Mwananchi Digital ofisini kwake jana, Meneja wa Tarura wilayani hapa Mhandisi Oscar Mussa alisema, tayari serikali imetoa idhini ni ya kufanya matengenezo yanayofikia  Sh672 milioni zitakazojenga madaraja manne ambapo madaraja matatu kati ya hayo manne yatakengwa katika barabara ya Mipera - Mikaranga – Ilela na moja litajengwa barabara ya Mitawa –Ilela.

“Madaraja haya yanaupana tofauti, madaraja mawili ni ya mita 10, na daraja moja ni  la mita 12 la nne ni la mita tano, pia tutaziba mashimo yaliyotokea kwa sababu ya mmomonyoko wa ardhi, tutajenga mitaro na kuweka kifusi katika maeneo mbalimbali ya barabara hizo, tumepima ili kujua vizuri aina ya ujenzi unaotakiwa,” alisema Mhandisi Oscar.

Alisema walikuwa na dharula barabara ya Mapera - Mikaranga - Ilela ambayo ina kilometa 13.9 barabara ya Mitawa –Ilela yenye urefu wa kilometa 7.24  ambayo inafanya jumla ya urefu wa barabara hizo kuwa kilometa 21.2 ambazo zilipata madhara ya kuharibiwa na Mvua.

Aidha amewataka wanachi wa vijiji hivyo kuendelea kuwa wavumilivu wakati  serikari kupitia Tarura inaendelea kufanya ukarabati  wa barabara hizo.

Naye Adrian Haule ameishukuru serikali kwa kuwajali wananchi na kuanza ukarabati huo ambao ni muhimu kwani barabara zimejifunga kutokana na kuharibika kwa madaraja na kusababisha kero kubwa kwa wananchi.