Mvua yasababisha JPM achelewe kuzindua kiwanda -VIDEO
Muktasari:
Uzinduzi wa kiwanda hicho ulipangwa kufanyika saa nne asubuhi, lakini mvua iliyonyesha kwa zaidi ya saa moja imechelewesha uzinduzi huo
Morogoro. Mvua kubwa iliyonyesha kwa saa moja imefanya shughuli ya uzinduzi wa kiwanda cha sigara cha Philip Moris zichelewe kuanza, huku wananchi mkoani Morogoro wakikubali kulowa kwa ajili ya kumsubiri Rais John Magufuli kufika kiwandani hapo.
Wananchi na viongozi waliohudhuria katika uzinduzi huo walianza kuwasili katika viwanja hivyo leo Alhamisi Machi 15,2018 kuanzia saa 2 asubuhi.
Pamoja na kunyesha mvua kubwa hali ya ulinzi umeimarishwa katika viwanja hivyo na baada ya kukatika, shughuli hizo za uzinduzi ziliendelea kama zilivyopangwa.