Mwalimu afungwa miaka 30 jela kwa kumbaka mwanafunzi wake Mufindi

Muktasari:

  • Pia Mahakama imetoa amri kwa mshtakiwa kumlipa fidia ya Sh5 milioni muhanga huyo.

Mufindi. Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, imemuhukumu kifungo cha Miaka 30 Jela Mwalimu Onesmo John Sanga (51) wa Shule ya Sekondari Kibengu iliyopo wilayani hapa baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wake  na kumpatia ujauzito (17).

Kesi hiyo ya jinai namba 28 ya mwaka 2023 ambayo hukumu yake imetolewa Mei 23, 2023  na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Benedict Nkomola. 

Sanga alitenda kosa hilo Februari 12 na Novemba 6, 2022 huko maeneo ya  Kijiji cha Kibengu, K ata ya Usokame Wilaya Mufindi kwa kutenda kosa hilo huku Mahakama ikamtia hatiani kwa makosa mawili ya ubakaji chini ya kifungu cha sheria 130 (1)(2)(e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la Mwaka 2022.

Aidha ilielezwa mahakamani hapo, mshtakiwa alikuwa akimdanya Mwanafunzi huyo kwa kumpatia fedha ya Sh10,000 baada ya kufanyia ubakaji huo huku akimwahidi kumsaidia katika masomo yake.

Inadaiwa kuwa sababu ambayo imepelekea mshtakiwa kufikishwa mahakamani hapo ni baada ya mwalimu huyo kumpa ujauzito mwanafunzi wa wa kidato cha tatu wa shule hiyo hali ambayo ilisababisha mwanafunzi huo kuumwa baada ya kupewa dawa kwa ajili ya kutoa ujauzito huo.

" Muhanga aligundulika na baba yake mzazi baada ya  kuumwa kutokana na  dawa ambazo alipewa na mshtakiwa na kuzitumia kwa ajili ya kutoa ujauzito huo hali ambayo imepelekea mhanga huyo kusema ukweli kwamba    ujauzito huo alipewa na mwalimu wake,"amesema mwathirika huyo.

Mshtakiwa baada ya kusomewa shitaka lake alikiri kufahamu  Mwanafunzi huyo kwa madai  kwamba anamfundisha somo la Biolojia katika darasa  la mwanafunzi huyo, huku akidai kwamba madai ya kesi hiyo si ya kweli bali amesingiziwa kutokana na chuki za kisiasa.

Awali akizungumza kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakari wa Serikali, Yahaya Misango amesema kuwa kesi hiyo ilikuwa na mashahidi watatu ambao ni mwathirika, baba mazazi wa mwathirika  pamoja na daktari ambaye amefanyia uchunguzi wa tukio hilo.

Pia, misango ameiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kea mashtakiwa kwakuwa matukio hayo hasa ya walimu kubaka wanafunzi kuongezeka katika Wilaya ya Mufindi na Tanzania kwa ujumla.

" Niombe mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa kutoka na vitendo hivi hasa vya walimu kubaka wanafunzi wao kuongezeka kila kilicha wilayani hapa na Tanzania kwa ujumla na ukizingatia walimu wamepewa dhamana kubwa ya kuwalinda na kuwafundisha maadili mema watoto Pindi wanapokuwa shuleni," amesema Misango.

Hata hivyo mahakama hiyo imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela ambapo adhabu hiyo itaenda sambamba kwa makosa yote mawili huku ikitoa amri kwa mshtakiwa kumlipa fidia ya Sh5 milioni mwathirika huyo.