Mwili wa Magufuli wawasili Chato

Magufuli kupitishwa daraja la JPM Kigongo-Busisi

Muktasari:

  • Maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wamemiminika  uwanja wa ndege jijini humo kupokea mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam.

Maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wamemiminika  uwanja wa ndege jijini humo kupokea mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam.

Baada ya kupokewa, msafara utakwenda uwanja wa CCM Kirumba ambako wakazi wa Mwanza na mikoa jirani watatoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo.

Baada ya kuagwa, msafara wa mwili wa Hayati Magufuli utazunguka mitaa mbalimbali ya Jiji hilo ambako wananchi waliokosa fursa ya kuaga uwanjani watafanya hivyo kwa kujipanga pembezoni mwa barabara.

Ukiwa njiani kupelekwa nyumbani kwake Chato mkoani Geita, mwili wa Hayati Magufuli utapitishwa mitaa ya Igogo, Mkuyuni, Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Nyashishi, Usagara, Kigongo na kuvuka hadi Busisi wilayani Sengerema.