Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwinyi: Nyaraka ziandaliwe kwa Kiswahili

Rais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi akizungumza katika kilele cha siku ya Kiswahili Duniani iliyofanyika ukumbi wa Chuo Cha Polisi Zanzibar leo Julai 7, 2023.

Unguja. Rais Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amesema ili kuendeleza, kukuza na kueneza Kiswahili ni vyema kuandaa machapisho na kutayarisha nyaraka zote za kiutendaji kwa lugha hiyo.

Dk Mwinyi ameeleza hayo leo Julai 7, 2023 alipomuwakilisha Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Kiswahili duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Polisi Ziwani, Zanzibar.

“Lengo ni kuhakikisha tunaongeza misamiati na kukitangaza na kukieneza zaidi Kiswahilim,” amesema

Kadhalika, amesema taasisi za kuendeleza na kukuza lugha hiyo kwa kushirikiana na vyuo vikuu zina wajibu wa kuhakikisha wanapatikana wataalamu wa kutosha waliomahiri katika kukidhi matarajio hayo.

Akizungumzia kauli mbiu ya siku hiyo inayosema ‘Kiswahili chetu Umoja wetu’ amesema ni vyema kuendelea kuonyesha umoja katika kutumia Kiswahili kwa ufasa ili wengine waweze kujifunza kutoka kwao.

Amesema pia ni vyema kujitahidi kufuatilia na kuzitumia fursa za Kiswahili zilizomo ndani ya nje ya nchi kwani mahitaji ya lugha hiyo duniani yanaendelea kuongezeka kila siku.

Naye Waziri Habari, Vijana, Sanaa na Michezo, Tabia Maulid Mwita, amesema pamoja na mambo mengine wanendelea kusimamia sera na sheria zilizowekwa katika mabaraza ya Kiswahili ili kukikuzaza na kukieneza Kiswahili kiwe bidhaa na kuleta pato kwa taifa.

Naye Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Pindi Chana alisema harakati za ukombozi zilizofanywa na wasisi wa taifa hili zilifanyika kwa lugha ya Kiswahili na ushirikiano katika jamii unachangiwa na kukuwa kwa lugha ya Kiswahili.

Awali mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa la Sayansi Elimu na Utamaduni (Unesco), Michael Tatoo amesema Kiswahili ndio lugha pekee ya kiafrika ambayo sio tu imepewa siku yake, bali ndio lugha pekee ya kiafrika ambayo imewezwa kuingizwa kwenye mifumo ya kompyuta hivyo kasema kunahitajika jitihada za makusidi kukuza lugha hiyo kwa njia ya digitali.

“Tunahitaji kujifunza zaidi lugha hii, mana ni lugha ya amani, inaleta umoja na kuwezesha mazungumzo na kuimarisha ushirikiano katika Bara la Afrika,” amesema

Kabla ya kufikia kilele chake leo, maadhimisho hayo yalitanguliwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbio za marathon, jukwaa la wahariri, mjadala wa wazi na kongamano la wanafunzi wa sekondari lengo ni kukitangaza na kuitambulisha siku hiyo ya kiswahili ambayo ilitangazwa Novemba mwaka jana na Unesco kuwa kila Julai 7 itakuwa siku maalumu.