Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nassari awafunda viongozi wa dini nchini

Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari

Muktasari:

Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo wakati wa ibada ya kustaafu kwa Askofu Paulo Akyoo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Meru Jimbo la Mashariki ambaye nafasi yake imechukuliwa na Askofu Elias Nasari, Diwani wa Kikatiti, Elisa Mungure amesema amani ni muhimu katika Taifa lolote duniani.

Moshi. Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari amesema viongozi wa dini wana wajibu wa kuhakikisha amani ya nchi haitoweki.

Akizungumza kwa niaba ya mbunge huyo wakati wa ibada ya kustaafu kwa Askofu Paulo Akyoo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Meru Jimbo la Mashariki ambaye nafasi yake imechukuliwa na Askofu Elias Nasari, Diwani wa Kikatiti, Elisa Mungure amesema amani ni muhimu katika Taifa lolote duniani.

Amesema mfumo wa maisha ya binadamu katika kufikia malengo anayojiwekea, unategemea uwapo wa utulivu.

Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Fredrick Shoo amekemea tabia ya watu kufanya biashara ya binadamu na uuzaji wa dawa za kulevya, kwani kufanya hivyo wanaipeleka nchi pabaya.

Dk Shoo akasema matukio hayo hayampendezi Mungu na yamekuwa yakisababisha madhara makubwa kwa jamii.

“Jamii hivi sasa imeharibika, kuna kila aina ya uhalifu unaofanywa kutokana na umaskini, naomba watu wafanye biashara halali kwani hayo yote yanafanyika kutokana na kukosa neema ya Mungu,” amesema Dk Shoo.