Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zahimizwa kuondoa vikwazo vya biashara

Muktasari:

  • Changamoto za kikodi, utekelezaji duni na ukosefu wa ulinganifu wa sera vinatajwa kama baadhi ya vikwazo vikwazo vya ufanyanyaji wa biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dar es Salaam. Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zahimizwa kuondoa vikwazo katika upande wa usafirishaji wa bidhaa ili kuimarisha biashara na ukuaji wa uchumi katika ukanda huo.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Elias Lukumay wakati wa mkutano wa wadau wa usafirishaji Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Lukumay amebainisha baadhi ya vikwazo hivyo kuwa ni changamoto za kikodi, utekelezaji duni na ukosefu wa ulinganifu wa sera.

Amesema licha ya EAC kuwa soko la pamoja, bado kuna utofauti katika mfumo wa kodi na ushuru wa forodha.  

Ameeleza kuwa kila nchi mwanachama ina muundo wake wa kodi, jambo linalosababisha ukosefu wa uwiano katika sera za kibiashara.  

“Kwa sasa, viwango vya VAT vinatofautiana kati ya nchi wanachama wa EAC, Kukosekana kwa ulinganifu huu vinasababisha vikwazo kibiashara”alieleza.  

Vilevile, kanuni za mizani na ushuru zinatofautiana kati ya nchi nazo husababisha vikwazo katika usafirishaji wa bidhaa katika ukanda huo.

“Malori yanayosafirisha bidhaa kutoka Tanzania hukabiliwa na gharama tofauti za mizani yanapoingia katika nchi jirani, jambo linalosababisha gharama zisizotabirika kwa kampuni za usafirishaji”anaeleza.  

Ameongeza changamoto nyingine ambayo wangetamani ifanyiwe marekebisho kwa haraka ni kutofautiana kwa sera kati ya EAC na SADC.

Biashara nyingi za Tanzania zinategemea masoko ya SADC, lakini baadhi ya sera kati ya jumuiya hizi mbili zinapingana.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) Elias Lukumay.

Lukumay alitolea mfano kusafirisha mizigo  kutoka Afrika Kusini hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupitia Bandari ya Dar es Salaam ni ghali ikilinganishwa na bandari za mataifa mengine ya SADC kutokana na kutokulingana kwa sera za kibiashara.  

Kwa upande wake Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Machano Ali Machano, kanda hii imekuwa na sera na makubaliano yaliyojengwa kwa mifumo imara, lakini changamoto kubwa ipo katika utekelezaji.  

“Tatizo halisi ni utekelezaji. Tunazo sera nzuri, makubaliano madhubuti, na ahadi imara, lakini utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa,” alisema.  

Kaimu Mkuu wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS), Dk Patrick Mbwile, alisisitiza kuwa utatuzi wa changamoto hizo unahitaji ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wadau wengine muhimu katika ukanda huo.

Ikumbukwe kuwa miaka kumi na mitatu iliyopita, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) zilipanga kuanzisha eneo la biashara huria la pande tatu ili kuunda mazingira bora ya kibiashara katika kanda.