Ndugai: Waziri Mwambe ana majibu ya kifedhuli

Thursday April 08 2021
ndugaipic

Spika wa Bunge Job Ndugai

By Sharon Sauwa

Dodoma. Spika wa Bunge Job Ndugai amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wabunge kuhusu majibu aliyoyaita ya kifedhuli yanayotolewa na Waziri wa  Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geofrey Mwambe na kumtaka Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumfunda.

Ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 8, 2021 mara baada ya mbunge wa Singida Magharibi (CCM),  Elibariki Kingu kumlalamikia Mwambe  wakati akichangia Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa (2021/22 hadi 2025/26) kwamba alijibiwa vibaya na waziri huyo baada ya kutoa ushauri wakuhusu masoko.

“Ninayo malalamiko kadhaa kuhusu Waziri Mwambe. Nadhani kwa sababu ni mbunge mgeni anadhani kuwa ukiwa waziri ni mtu mkubwa sana bungeni haiendi hivyo. Ana majibu ya ovyo sana hawaheshimu hata wabunge wa kamati yake wanapata tabu jinsi ya kufanya naye kazi.”

“Haiwezekani ukimnyanyasa mbunge moja umenyanyasa wabunge wote, ukinyanyasa kamati moja umenyanyasa kamati zote. Duniani kote hakuna waziri anayemjibu fedhuli mbunge ni vizuri tumwachie mheshimiwa waziri mkuu ili akakae naye amfunde,” amesisitiza.

Advertisement