Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Necta yaleta mfumo mpya utunzaji taarifa za wanafunzi

Muktasari:

Msonde amesema mfumo huo  utawasajili wanafunzi wa shule za msingi  na kupewa namba maalumu watakazotumia ngazi zote za elimu.

Dar es Salaam. Baraza la la Mitihani la Tanzania (Necta), limezindua Mfumo wa Kutunza Taarifa za Wanafunzi wa Shule za Msingi (PRem), utakaowezesha baraza hilo kupata takwimu mbalimbali za usajili wa upimaji darasa la nne na kumaliza elimu ya msingi.

Mfumo huo umezinduliwa leo, Mei 5, 2018 na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Elimu, Sayansi  na Teknolojia,  Dk Leonard Akwilapo  na ulifanyika katika kituo cha kusahihisha mitihani, Mbezi.

Katika uzinduzi huo Katibu Mtendaji wa Nacte, Dk Charles Msonde amesema kupitia mfumo huo wanafunzi wa shule za msingi watasajiliwa na kupewa namba maalumu za utambulisho watakazotumia kwenye ngazi zote za elimu.

Amesema mfumo huo pia, utamwezesha mwanafunzi  kuhama shule moja kwenda nyingine ndani ya kata, halmashauri au mkoa na atakuwa akiidhinishwa kwa wakati na maofisa elimu kupitia PRem.

Kwa upande wake, Dk Akwilapo ameshukuru ubalozi  wa Sweden nchini kwa kufadhili mradi huo utakaosaidia kufuatilia taarifa za matokeo ya mwanafunzi katika ngazi ya shule, halmashauri, manispaa ya jiji, mkoa na kitaifa.

"Mfumo huu una umuhimu mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini.Sasa hivi wanafunzi wote wa shule za msingi watapatikana katika kanzidata moja,"amesema Dk Akwilapo.